Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-KAZI

Mageuzi ya pensheni: Bunge la Seneti laidhinisha, hatua ya mwisho ya uamuzi katika Bunge

Hali ya sintofahamu huenda ikaripotiwa nchini Ufaransa baada ya Bunge la seneti kuidhinisha mpango wa serikali wa mageuzi ya pensheni. Baraza la Bunge linatazamiwa kufanye uamuzi wa mwisho kuhusu mswada wa marekebisho ya pensheni, ambao unalenga hasa kusogeza mbele umri halali wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64.

Bunge la kitaifa linatazamiwa kupiga kura, Alhamisi, Machi 16, 2023, mradi wa mageuzi ya pensheni. kura itakayopigwa na wabunge wa Republican utakuwa muhimu kwa kambi ya rais.
Bunge la kitaifa linatazamiwa kupiga kura, Alhamisi, Machi 16, 2023, mradi wa mageuzi ya pensheni. kura itakayopigwa na wabunge wa Republican utakuwa muhimu kwa kambi ya rais. AP - Christophe Ena
Matangazo ya kibiashara

Haishangazi, maseneta walipitisha nakala iliyojadiliwa katika kamati ya pamoja. Lakini katika Baraza la Bunge la Kitaifa, huenda mageuzi haya yakarudishwa nyuma, kwani ni taasi ambayo inadhibitiwa na upinzani. Na Warepublican bado wana hatima ya mageuzi haya mikononi mwao.

Mkutano wa mwisho wa kundi ulioandaliwa Jumatano jioni katika Bunge la Kitaifa kufafanua misimamo ya kila upande hautakuwa na manufaa mengi. Kulingana na washirika wa karibu wa Olivier Marleix, kiongozi wa kundi la Warepublicain katika makao makuu ya Baraza la Bunge, Bourbon, kati ya wabunge 34 na 36 kwa jumla ya wabunge 61 wana uhakika wa kupiga kura kwa ajili ya mageuzi ya pensheni.

Swali muhimu ni nini wengine watafanya: je, watakataa, watapiga kura ya kupinga?  Kwa sababu kwa kambi ya rais, kila kura inahesabiwa, na ni bora kwa mfano kutopiga kura kuliko kura moja zaidi dhidi ya nakala hii, anaeleza Pierrick Bonno, wa kitengo cha Siasa cha RFI.

Majadiliano ya kamati ya pamoja juu ya taaluma ndefu hasa hayajashawishi wengi. Wabunge watatu au wanne tu ndio wanaweza kubadilisha kura zao, kulingana na chanzo cha bunge. Lakini baadhi ya wabunge kutoka chama cha LR wanakusudia kuficha kadi zao hadi dakika ya mwisho.

"Tutadumisha hali hiyo isiyo wazi hadi wakati wa kupiga kura. Kwa sababu lengo letu si 49-3, ni kushinikiza serikali kuchukua hatari ya kuandaa kura ili isifaulu, "anasema mshirika wa karibu wa Mbunge Aurélien Pradié. Mchezo wa uwongo utaendelea hadi mwisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.