Pata taarifa kuu

Shinikizo zaidi kwa serikali ya rais Macron kuhusu muswada wa pensheni

NAIROBI – Rais wa Ufaransa, hapo jana ametoa wito wa utulivu wakati huu akitumai kuwa mabadiliko ya sera ya Pensheni aliyoyapitisha bila bunge mchakato wake utakamilika, matamshi anayotoa saa chache kabla ya bunge kupiga kuta ya kuwa na Imani na Serikali yake au la.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron AP - Michel Euler
Matangazo ya kibiashara

Muswada huu wa sheria wenye utata, ambao umesababisha miezi kadhaa ya maandamano ya raia na kupingwa katika bunge, unatarajiwa kupitishwa na bunge hivi leo lakini utategemea kama kura ya kutokuwa na imani na Serikali yake itaungwa mkono au la.

Katika tarifa yake, Macron, amesema ni matarajio yake kuona mapendekezo yake yakiungwa mkono na kupitishwa, akikiri kuelewa wasiwasi walionao wafanyakazi.

Ikiwa muswada huu utapitishwa, utaruhusu kuongezwa kwa umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64 pamoja na muda ambao wafanyakazi watatakiwa kulipa katika mfumo ili waje kupokea malipo yao yote ya kiinua mgongo.

Hata hivyo licha ya wito Wake, maandamano zaidi yanatarajiwa hivi leo kuweka shinikizo kwa muswada huo kuondolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.