Pata taarifa kuu

Mageuzi ya pensheni nchini Ufaransa: Watu 310 wakamatwa katika maandamano

Jumla ya watu 310 walikamatwa Alhamisi nchini Ufaransa, wakiwemo 258, mjini Paris wakati wa maandamano ya kupinga kupitishwa kwa mpango wa serikali wa mageuzi ya pensheni bila kupigiwa, maandamano ambayo yameendelea Ijumaa asubuhi na kuzuiwa kwa muda kwa moja ya barabara kuu mjini Paris.

Waandamanaji walikusanyika katika eneo la Place de la Concorde, karbu na makao makuu ya Bunge la Kitaifa mjini Paris, baada ya uamuzi wa serikali kutumia kifungu cha 49.3 cha Katiba kupitisha mageuzi ya pensheni, Alhamisi Machi 16, 2023.
Waandamanaji walikusanyika katika eneo la Place de la Concorde, karbu na makao makuu ya Bunge la Kitaifa mjini Paris, baada ya uamuzi wa serikali kutumia kifungu cha 49.3 cha Katiba kupitisha mageuzi ya pensheni, Alhamisi Machi 16, 2023. AP - Thomas Padilla
Matangazo ya kibiashara

Katika miji mingine 24, watu 52,000 walishiriki katika maandamano, kulingana na polisi.

"Upinzani ni halali, maandamano ni halali, vurugu au uchochezi wa vurugu hapanai," Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Gérald Darmanin amesema leo Ijumaa kwenye RTL, akitangaza idadi ya watu 310 waliokamatwa. 

Polisi waliingilia kati mapema Alhamisi jioni kwenye eneo la Place de la Concorde, karibu na makao makuu ya Bunge la Kitaifa, lililokaliwa na maelfu ya waandamanaji wanaopinga mageuzi ya pensheni.

Huko Paris watu 10,000 walikusanyika katika uwanja, ulio karibu na Bunge la Kitaifa, kulingana na Gérald Darmanin. Katika miji mingine 24, watu 52,000 walishiriki katika maandamano Alhamisi jioni, kulingana na polisi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameamua kulazimisha kuuidhinisha mpango wake wa mageuzi ya pensheni bila kuitisha kura bungeni.

Vyanzo kadhaa vilivyo karibu na ofisi ya rais vimeliambia shirika la habari la AFP kwamba kiongozi huyo atatumia uwezo wa kikatiba unaoiwezesha serikali kuwapiku wabunge.

Rais Macron amechagua kutumia kifungu cha 49.3 cha katiba ya Ufaransa baada ya mikutano kadhaa na viongozi wakuu, akiwemo Waziri Mkuu Elisabeth Borne, baada ya kubaini kwamba hakukuwepo na wabunge wengi wa kupitisha mageuzi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.