Pata taarifa kuu

Ufaransa-Uingereza: Ufadhili wa kituo cha kuwazuilia wahamiaji wakosolewa

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak katika ziara yake siku ya Ijumaa Machi 10 nchini nchini Ufaransa aliiandamana na mawaziri saba, kama sehemu ya mkutano wa kilele kati ya Ufaransa na Uingereza, ikiwa ni mkutao wa kwanza katika kipindi cha miaka mitano.

Wahamiaji wakitokea nchini Ufaransa wanajaribu kuvuka Bahari kwenda Uingereza, Machi 15, 2022.
Wahamiaji wakitokea nchini Ufaransa wanajaribu kuvuka Bahari kwenda Uingereza, Machi 15, 2022. © Sameer al-Doumy / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mgeni wake wa heshima walizungumza kuhusu mabadilishano ya kitamaduni au ushirikiano wa kijeshi. Sera ya uhamiaji imechukua nafasi muhimu, pamoja na makubaliano mapya ambayo yamekosolewa na mashirika yasiyo ya kiserikali.

London itatao euro milioni 540 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo ili kuzuia wahamiaji kuvuka bahari kuingia katika nchi hizo. Mradi huu haujapokelewa vizuri huko London. Makubaliano ya Ijumaa hii yanaruhusu ujenzi wa kituo cha kuwazuilia wahamiaji huko Hauts-de-France. Mbinu hii inakemewa na mashirika yasiyo ya kiserikali. Kwa upande wa shirka la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International, kwa mfano, inasema Uingereza iinakwepa majukumu yake'.

►Soma pia: London kufadhili kituo cha kuwazuilia wahamiaji nchini Ufaransa

Zoe Gardner, mwanachama wa shirika la wakimbizi, anakosoa kwenye televiseni ya Sky News kiini cha mkakati huo. "Madhumuni ya kuwekwa kuwazuia wahamiaji ni ya kiutawala, ni kumweka mtu mahali pamoja wakati wa kuandaa kumfukuza, amebaini. Hata hivyo, watu ambao wako kwenye pwani ya Ufaransa wanatoka nchi ambazo itakuwa hatari kuwarudisha, na kwa hivyo itakuwa kinyume cha sheria. Na Wafaransa hawana uwezo wa kuwafukuza, acha sisi! "

'Wahamiaji wengi zaidi wanateseka'

Chama cha upinzai cha Labour kinataka kurejeshwa kwa wahamiaji nchini Ufaransa. Zoe Gardner pia anaonyesha kutofaulu kwa aina hii ya makubaliano. “Mwaka jana pekee, Waziri wa Mambo ya Ndani alitoa euro milioni 80 kwa mwaka kujenga uzio zaidi na kuandaa doria zaidi nchini Ufaransa. Na hii ni mfano mmoja tu kati ya mfululizo mzima wa mikutano mingine na makubaliano mengine, ambapo kitita cha pesa kinalipwa kwa Ufaransa, na hakuna kinachobadilika, isipokuwa kwamba wahamiaji wengi zaidi wanateseka. "

Wachambuzi wanatarajia watu 80,000 kuvuka Bahari kwa kutumia boti mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.