Pata taarifa kuu

Rais Macron akutana na waziri mkuu wa Uingereza Sunak

NAIROBI – Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amekutana na mwenyeji wake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron jijini Paris, katika kikao muhimu cha kujadili uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak AP - Kin Cheung
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa masuala yanayojadiliwa na viongozi hao wawili ni namna ya kupata suluhu ya kudumu kuhusu wahamiaji haramu wanaotumia usafiri wa majini kutaka kufika katika nchi hizo mbili, lakini pia ushirikiano wa kibishara baada ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Ripoti iliyochapishwa katika Gazeti la The Times, zinasema Uingreza imeilipa Ufaransa Euro Milioni 225 kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo ili iisadie kuzuia wahamiaji haramu kufika katika nchi yake kwa kupiga doria za mara kwa mara kwenye mkono wa Bahari unaounganisha nchi hizo mbili.

Sunak ameelezea ziara yake jijini Paris kama, hatua muhimu itakayoimarisha zaidi uhusiani kati ya nchi hizo mbili, ambazo kwa kipindi kirefu zimeshindwa kuafikiana kuhusu namna ya kushughulikia wahamiaji haramu.

Huu ni mkutano wa kwanza kati ya viongozi wa Ungereza na Ufaransa kwa kipindi cha miaka mitano.Mawaziri wakuu wawili waliopita wa Uingereza, walionekana kuwa na uhusiano baridi na Macron.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.