Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-KAZI

Ufaransa kukumbwa na maandamano makubwa dhidi ya mageuzi ya pensehi

Maandamano makubwa yanatazamiwa kufanyika Jumanne hii Mach 7 nchini kote Ufaransa, kupinga mageuzi ya pensheni, mradi unaoendelea kujadiliwa katika Baraza la Seneti nchini humo.

Siku hii ya maandamano ni ya sita dhidi ya mageuzi haya ya pensheni.
Siku hii ya maandamano ni ya sita dhidi ya mageuzi haya ya pensheni. AP - Christophe Ena
Matangazo ya kibiashara

Ili "kuiweka Ufaransa katika hali ya sintofahamu" Jumanne hii, Machi 7, muunganowa vyama vya wafanya kazi unategemea maandamano makubwa na mgomo wa jumla katika sekta nyingi, na hilo ndio lengo kubwa la muungano huo.

Muungano wa vyama vya wafanyakazi unaahidi kuhamasisha sekta zote kujiunga katika maandamano makubwa na mgomo wa jumla ili kushinikiza serikali kuachana na mpango wake wa mageuzi ya pensheni. Muungano huo CGT unasema maanamano hayo "yatakuwa ya kipeke na yasiyosahaulika". Wakati mradi wa mageuzi ya pensheni unaendelea kujadiliwa katika Baraza la Seneti, CGT inakusudia kufanya Jumanne hii, Machi 7 kuwa siku ambayo hakuna hata shughuli moja itakayofanyika nchini Ufaransa. Miungano ya vyama vya CGT na Solidaires tayari wameitisha mgomo usiokoma na ambao utaendelea hadi pale serikali itatekeleza madai yao. Kulingana na kura ya maoni ya mapema mwezi huu, 72% ya Wafaransa wanapinga mswada huo, dhidi ya 66% mwezi Januari.

Katika sekta ya usafiri, shughuli katika shirika la reli nchini Ufaransa "zitazorota sana" siku ya Jumanne. Vyama vya wafanyakazi vya TGV na TER, viko tayari kujiunga katika maandamano hayo.

Kurugenzi Kuu ya Usafiri wa Anga (DGAC) imezitaka kampuni kupunguza ratiba zao za usafiri siku za Jumanne na Jumatano, kwa 20% huko Paris-Charles-de-Gaulle na kwa 30% huko Paris-Orly, Beauvais, Bordeaux, Lille, Lyon, Nantes, Marseille, Montpellier, Nice na Toulouse.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.