Pata taarifa kuu

Ufaransa: Siku ya nne ya maandamano ya Ufaransa kupinga marekebisho ya pensheni.

Maandamano ya nne yamefanyika kote nchini Ufaransa, kuendelea kupinga mageuzi ya rais Emmanuel Macron kuhusu mfumo wa pensheni na kuongeza umri wa wafanyakazi kustaafu kutoa miaka 62 hadi 64.

Waandamanaji waliandamana wakati wa maandamano huko Paris mnamo Februari 11, 2023, ikiwa ni pamoja na mwanamume akionyesha bango linalosema "Sikiliza hasira za watu".
Waandamanaji waliandamana wakati wa maandamano huko Paris mnamo Februari 11, 2023, ikiwa ni pamoja na mwanamume akionyesha bango linalosema "Sikiliza hasira za watu". © RFI
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yamepangwa na vyama vya wafanyakazi nchini humo na wanasiasa wanaompinga rais Macron.

Siku ya Jumanne maandamano mengine yalifanyika nchini humo, lakini hayakuhudhiriwa na watu wengi kama ilivyokuwa ya leo, kutokana na kupata uungwaji mkono wa wanafunzi na watu wengine ambao hawakujitokeza mapema wiki hii.

Mbali na maandamano na mgomo wa leo, uongozi wa vyama vya wafanyakazi, umepanga maandamano mengine Alhamisi ijayo, kuendelea kumshikiza rais Macron kuachana na mpango huo.

Aidha, maandamano mengine yamepangwa Machi tarehe 7 na 8, wakati Maseneta watakapokuwa wanajadili mageuzi hayo, huku wakionya maandmano na migomo zaidi iwapo serikali haitasikia kilio chao.

Rais Macron amesisitiza kuendelea na mageuzi hayo anayosema, yatatoa nafasi kwa wafanyakazi nchini Ufaransa kufanya kazi kwa zaidi na kulipwa malipo yao yote wanapostaafu, wanapotimiza miaka 64.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.