Pata taarifa kuu

Maandaamano zaidi yashuhudiwa nchini Ufaransa kupinga mageuzi ya pensheni

Maandamano ya nne yamefanyika kote nchini Ufaransa, kuendelea kupinga mageuzi ya rais Emmanuel Macron kuhusu mfumo wa pensheni na kuongeza umri wa wafanyakazi kustaafu kutoa miaka 62 hadi 64.

Waandamaji katika mji wa  Toulouse, Kusini mwa Ufaransa   Februari 11, 2023.
Waandamaji katika mji wa Toulouse, Kusini mwa Ufaransa Februari 11, 2023. AFP - CHARLY TRIBALLEAU
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa vyama vya wafanyazi, umepanga maandamano hayo, wakiungwa mkono na wanasiasa  wanaompinga rais Macron.

Siku ya Jumanne maandamano mengine yalifanyika nchini humo, lakini hayakuhudhiriwa na watu wengi kama ilivyokuwa siku ya Jumamosi, kutokana na kupata uungwaji mkono wa wanafunzi na watu wengine ambao hawakujitokeza mapema wiki hii.

Mbali na maandamano na mgomo wa leo, uongozi wa vyama vya wafanyakazi, umepanga maandamano mengine Alhamisi ijayo, kuendelea kumshikiza rais Macron kuachana na mpango huo.

Aidha, maandamano mengine yamepangwa Machi tarehe 7 na 8, wakati Maseneta watakapokuwa wanajadili mageuzi hayo, huku wakionya maandmano na migomo zaidi iwapo serikali haitasikia kilio chão.

Rais Macron amesisitiza kuendelea na mageuzi hayo anayosema, yatatoa nafasi kwa wafanyakazi nchini Ufaransa kufanya kazi kwa zaidi na kulipwa malipo yao yote wanapostaafu, wanapotimiza miaka 64.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.