Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-KAZI

Pensheni: Zaidi ya watu milioni 2.5 waandamana nchini Ufaransa, kulingana na CGT

Zaidi ya watu milioni 2.5 wameandamana nchini Ufaransa Jumamosi Februari 11 kupinga mageuzi ya rais Emmanuel Macron kuhusu mfumo wa pensheni na kuongeza umri wa wafanyakazi kustaafu kutoa miaka 62 hadi 64, kulingana na muungano wa mashirika ya wafanyakazi, CGT, wakati Wizara ya Mambo ya Ndani imebaini kwama watu 963,000 wameandamana.

Maandamano mengine yamepangwa Machi tarehe 7 na 8, wakati Maseneta watakapokuwa wanajadili mageuzi hayo, huku wakionya maandmano na migomo zaidi iwapo serikali haitasikia kilio chão.
Maandamano mengine yamepangwa Machi tarehe 7 na 8, wakati Maseneta watakapokuwa wanajadili mageuzi hayo, huku wakionya maandmano na migomo zaidi iwapo serikali haitasikia kilio chão. AP - Michel Euler
Matangazo ya kibiashara

Takwimu iliyotolewa na kituo cha vyama vya wafanyakazi ni chini ya ile ya Januari 31 (milioni 2.8). ), lakini juu zaidi kuliko ile ya Januari 19 na Februari 7 (karibu milioni 2).

Maandamano yalianzia katika mji wa Nancy na kisha mashariki mwa nchi huko Strasbourg na baadae Toulouse ambapo vyama vya wafanyakazi vmeonya kuwa viko tayari kuzuia shughuli zote nchini Ufaransa katika wiki zijazo ikiwa maombi yao hayatosikika.

Hii ni mara ya nne katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja ambapo Wafaransa wametakiwa kuandamana dhidi ya mageuzi hayo ya uongozi wa Rais Emmanuel Macron ambaye amesema kuwa mageuzi hayo ni muhimu ili kudumisha uwezo wa mfumo wa pensheni nchini Ufaransa.

Muungano wa vyama vya wafanyazi, umepanga maandamano hayo, wakiungwa mkono na wanasiasa  wanaompinga rais Macron.

Siku ya Jumanne maandamano mengine yalifanyika nchini humo, lakini hayakuhudhiriwa na watu wengi kama ilivyokuwa siku ya Jumamosi, kutokana na kupata uungwaji mkono wa wanafunzi na watu wengine ambao hawakujitokeza mapema wiki hii.

Mbali na maandamano na mgomo wa leo, uongozi wa vyama vya wafanyakazi, umepanga maandamano mengine Alhamisi ijayo, kuendelea kumshikiza rais Macron kuachana na mpango huo.

Aidha, maandamano mengine yamepangwa Machi tarehe 7 na 8, wakati Maseneta watakapokuwa wanajadili mageuzi hayo, huku wakionya maandmano na migomo zaidi iwapo serikali haitasikia kilio chao.

Rais Macron amesisitiza kuendelea na mageuzi hayo anayosema, yatatoa nafasi kwa wafanyakazi nchini Ufaransa kufanya kazi kwa zaidi na kulipwa malipo yao yote wanapostaafu, wanapotimiza miaka 64.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.