Ufaransa, vyama vya wafanyikazi kushiriki migomo zaidi wiki ijayo
Nchini Ufaransa, vyama vya wafanayazi, vimetangaza migomo mingine miwili wiki ijayo kuendelea kupinga sera ya Pensheni ya Serikali ya rais Emmanuel Macron.
Imechapishwa:
Cheza - 00:28
Jumanne, shughuli za masomo, usafiri na huduma nyingine za umma nchini zilitatizika kufuatia hatua ya maelfu ya wafannyakazi kujitokeza katika miji mbalimbali kupinga mpango wa rais Macron, kupinga ongezeko la umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64.
Aliyekuwa mgombea urais, mwaka uliopita Jean-Luc Mélenchon aliungana na waandamanaji kupinga mabadiliko hayo.
“Bila shaka rais Macron anapoteza kila ambacho anafanya ni kutupotezea muda.”ameeleza Jean-Luc Mélenchon.
Rais Emmanuel Macron, amesisitiza kuwa hatabadili msimamo wake licha ya maandamano yanayoendelea.