Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Vladimir Putin: Uhusiano wa Urusi na China 'unaimarisha hali ya kimataifa'

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema Jumatano hii, Februari 22 kwamba uhusiano wa Urusi na China 'unamarisha hali ya kimataifa", kwa mashaka kamili kuhusu mpango wa amani wa China kwa Ukraine, unaopaswa kuwekwa wazi wiki hii.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi (kushoto) akiwa na Vladimir Putin kwenye Ikulu ya Kremlin mjini Moscow Februari 22, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi (kushoto) akiwa na Vladimir Putin kwenye Ikulu ya Kremlin mjini Moscow Februari 22, 2023. AP - Anton Novoderezhkin
Matangazo ya kibiashara

"Uhusiano wa kimataifa ni mgumu leo ​​(...) Katika muktadha huu, ushirikiano (...) kati ya China na Urusi ni muhimu zaidi kwa utulivu wa hali ya kimataifa", amesema rais wa Urusi, alipokuwa anamkaribisha mkuu wa diplomasia ya China, Wang Yi katika ikulu ya Kremlin.

Vladimir Putin mara chache hupokea maafisa wa kigeni ambao sio wakuu wa nchi, mkutano huu kwa mara nyingine tena unasisitiza uhusiano wa upendeleo kati ya Kremlin na mshirika wake, China. "Tunafikia upeo mpya", amemkaribisha Vladimir Putin, na kuongeza kutarajia Rais wa China Xi Jinping pamoja na ziara yake nchini Urusi, inayotarajiwa katika majira ya joto.

Kwa upande wake, Wang Yi ameelezea nia ya Beijing ya "kuimarisha ushirikiano wa kimkakati (...) na ushirikiano wa pande zote" na Moscow, kulingana na maneno yake yaliyotafsiriwa kwa Kirusi. "Uhusiano wa Urusi na China "hauelekezwi dhidi ya nchi za ulimwengi wa tatu na kupinga shinikizo lao," amesisitiza.

China, mpatanishi katika mgogoro wa Ukraine?

Mkuu wa diplomasia ya China amepokelewa katika Ikulu ya Kremlin, baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov. "Mahusiano yetu yanaendelea kwa njia salama na yenye nguvu. Na licha ya misukosuko mikali duniani, tunaonyesha umoja, hamu ya kutetea masilahi ya mtu mmoja na mwingine, "amesema Sergei Lavrov wakati wa mkutano huu.

Ziara ya Wang Yi nchini Urusi inakuja wakati China inataka kuchukua nafasi ya upatanishi katika mzozo wa Ukraine kwa kuibua hadharani mpango wa amani - kwa wakati ambao haueleweki - kutafuta suluhisho la kisiasa. Wang Yi aliwasili Moscow siku ya Jumanne, baada ya kukutana wiki iliyopita na mkuu wa diplomasia ya Ukraine Dmytro Kouleba wakati wa mkutano wa usalama ulioandaliwa mjini Munich, Ujerumani, ambapo aliwasilisha, kulingana na Kiev, "mambo muhimu ya mpango wa amani ya China" kwa Ukraine.

China imeahidi kuchapisha pendekezo lake la "suluhisho la kisiasa" wiki hii, kwa wakati wa kuadhimisha mwaka wa kwanza wa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 24, 2022. Mshirika wa karibu wa Urusi, China haijawahi kuunga mkono wala kukosoa hadharani kampeni ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine, huku ikielezea mara kwa mara uungaji mkono wake kwa Moscow dhidi ya vikwazo vya nchi za Magharibi. Lakini pia alitoa wito wa kuheshimiwa kwa uadilifu wa eneo la Ukraine, wakati Moscow inadai kunyakuliwa kwa mikoa mitano ya Ukraine.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.