Pata taarifa kuu

Urusi imetangaza kujiondoa kwa mkataba wa nyuklia kati yake na Marekani

Rais wa Urusi, Vladmir Putin, Jumanne ya wiki hii alitangaza nchi yake kujitoa kwa muda katika ushiriki wa mkataba wa nyuklia kati yake na Marekani wa New START, mkataba uliosaidia kumalizika kwa vita baridi baina ya nchi hizo.

Rais wa Urusi Vladmir Putin
Rais wa Urusi Vladmir Putin © via REUTERS / SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huu ulitiwa saini mwaka 2010, ambapo baadhi ya vipengele vya mkataba unazibana nchi hizo kutuma au kuandaa kwa namna yoyote ile silaha za nyuklia kwenye maeneo ya mipaka.

Kujiondoa kwa Urusi katika utekelezaji wa mikataba ya kimataifa, si taifa la kwanza kufanya hivyo, mataifa mengine yaliyowahi kuchukua hatua kama hii ni pamoja na;

Mwezi Novemba mwala 2016, rais Putin aliiondoa nchi yake katika kutekeleza mkataba unaotambua mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, hatua kama hii ikachukuliwa na Burundi Oktoba 2017 ambapo nayo ilijitoa kwenye mahakama hiyo.

Mei 2018, aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump, alitangaza kuitoa nchi yake kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran, huku Agost 2019 akitangaza pia kuiondoa nchi yake kwenye mkataba wa nyuklia na Urusi, akisema unatishia usalama wa taifa lake mkataba huu ulitiwa saiani mwaka 1987 kati ya rais Ronald Regan na Mikhail Gorbachev.

Aidha November 2020 Marekani ilijitoa pia katika mkataba wa kimataifa wa Mazingira wa Paris.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.