Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-ULINZI

Joe Biden ataka kuwahakikishia washirika wa NATO kutoka USSR ya zamani

Baada ya ziara yake huko Kyiv na hotuba yake huko Warsaw, Rais wa Marekani Joe Biden anaanza siku yake ya mwisho ya ziara yake katika Ulaya Mashariki. Ikiwa uungwaji mkono kwa Ukraine uligubika hotuba zake tangu kuwasili kwake Kyiv Jumatatu, Februari 20, leo Rais wa Marekani atatangaza kipaumbele kwa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO.

Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa hotuba yake huko Warsaw mnamo Februari 21, 2023.
Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa hotuba yake huko Warsaw mnamo Februari 21, 2023. AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

Katika siku ya leo, Joe Biden Jumatano hii atahutubia kuhudu mkakati ambao nchi za NATO mashariki zinapaswa kupitisha mbele ya Urusi na washirika wake. Atakutana na wanachama wa kundi la Bucharest, ambalo linazileta pamoja nchi tisa za upande wa mashariki wa NATO na ambazo, nyingi, zinashiriki mipaka na Urusi au Ukraine.

Ishara kubwa

Kufanya mkutano huu nchini Poland ni ishara. Kwenye mipaka ya mzozo huo, Wapoland wengi wanahisi kutishiwa na jeshi la Urusi ikiwa litajilazimisha nchini Ukraine. Lakini Joe Biden amekumbuka wakati wa hotuba yake Jumanne jioni jinsi alivyokuwa ameshikamana na Kifungu cha 5 cha mkataba wa NATO mbele ya umati wa watu wenye furaha: " Kama mwanachama akishambuliwa, basi Muungano wote unashambuliwa. ".

Wanajeshi wa Marekani

Mwishoni mwa majadiliano ya leo, inatarajiwa pia kuwa Marekani itachukua uamuzi wa kuweka wanajeshi wa kudumu katika ardhi ya Poland.

Kitu cha kuimarisha zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili ambazo zilionyesha urafiki wao mkubwa machoni pa ulimwengu wakati wa mchana Jumanne. Rais wa Marekani anapaswa kuruka alasiri hadi Washington.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.