Pata taarifa kuu

Munich: Macron atoa wito kwa Ulaya 'kuwekeza tena kwa kiasi kikubwa' katika ulinzi wao

Mkutano wa Munich umeanza Ijumaa hii, Februari 17 huko Bavaria. Mkutano huu muhimu katika nyanja ya usalama huleta pamoja kila mwaka kundi la watoa maamuzi. Miongoni mwa washiriki mwaka huu: Emmanuel Macron, Olaf Scholz, lakini pia wakuu wa diplomasia ya China na Marekani.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa hotuba katika Mkutano wa Usalama wa Munich (MSC) Ijumaa hii, Februari 17, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa hotuba katika Mkutano wa Usalama wa Munich (MSC) Ijumaa hii, Februari 17, 2023. AFP - ODD ANDERSEN
Matangazo ya kibiashara

Nchi ambayo haijawakilishwa katika mkutao huu ni Urusi. Rais wa Ukraine amezungumza kwa njia ya video, na mwenzake wa Ufaransa, pamoja na Kansela wa Ujerumani, wanashiriki mkutano huo moja kwa moja.

Urusi haiwezi na haipaswi kushinda vita na uvamizi wa Urusi lazima ushindwe: hivi ndivyo Emmanuel Macron amesema wakati wa hotuba yake katika Mkutano wa Usalama wa Munich.

Naye rais wa Ufaransa, ambaye alikuwa akizungumza baada ya matangazo ya ujumbe kutoka kwa mwenzake wa Ukraine, akiomba kuharakishwa kwa msaada kwa nchi yake, amesema: "Lazima tuzidishe msaada wetu. "

Lakini hakutoa matangazo mapya juu ya uwezekano wa usafirishaji wa silaha, kama anavyotaka Rais Zelensky , au uwezo wa kutumia ili kuwezesha Kiev kushinda.

Emmanuel Macron amesisitiza kwamba ni muhimu kujiandaa kwa amani, kwa kuwa na ujasiri wa kushiriki tena katika mazungumzo. Lakini ameongeza mara moja kwamba wakati huu sio wa mazungumzo kwa sasa.

Rais wa Ufaransa amehakikisha: “Tuko tayari kwa mzozo wa muda mrefu katika kukabiliana na ukweli wa mapigano ambayo ni makali kwenye uwanja wa vita. Kwa hivyo ametoa ujumbe unaokusudiwa pia kwa maoni ya umma wa Ufaransa: vita vya Ukraine vitadumu pamoja na athari zake katika maisha yao ya kila siku.

Rais wa Ufaransa pia amechukua fursa kwenye jukwaa la Mkutano wa Munich kukaribisha nchi za Ulaya kufikiria upya itikadi yao ya usalama. Pia ametangaza kuandaa mkutano wa ulinzi wa anga wa Ulaya, hivi karibuni jijini Paris.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.