Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Zelensky atoa ujumbe kwa nchi za Magharibi baada ya Ufaransa na Ujerumani kumuunga mkono

Baada ya ziara yake ya kushtukiza mjini London, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliwasili Paris Jumatano jioni Februari 8, na kupokelewa na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye pia alimwalika Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, rais Zelensky akitarajiwa kukutana na viongozi wa EU siku ya Alhamisi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, akiwa na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani pembeni yake, katika Ikulu ya Élysée Jumatano hii, Februari 8, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, akiwa na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani pembeni yake, katika Ikulu ya Élysée Jumatano hii, Februari 8, 2023. AP - Sarah Meyssonnier
Matangazo ya kibiashara

Rais Macron alishiriki chakula cha jioni na Zelensky na Scholz, kwa lengo la "kuthibitisha tena msaada usioshindwa" wa nchi hizi mbili kwa Ukraine, "na kuendelea na uratibu wa karibu ambao utawezesha kujibu kwa ufanisi kwa mahitaji yaliyotolewa na Kyiv", kulingana na ikulu ya Elysée.

Kulingana Viongozi hao watatu walizungumza na waandishi wa habari kabla ya kufanya mkutano wa faragha, kulingana na shirika la habari la AFP.

Siku ya Alhamisi, Volodymyr Zelensky anatarajia kufanya mazungumzo na viongozi wa Umoja wa Ulaya.

Katika ikulu ya Ufaransa, Emmanuel Macron alimhakikishia mwenzake wa Ukraine kuhusu nia yake ya kuendelea kusafirisha silaha za Ufaransa kwa Kyiv, akisema utawala wake  utaendeleza juhudi katika suala la utoaji wa uwezo wa ulinzi. 

Ziara yako ya Paris jioni hii ni fursa kwetu kwanza kutoa heshima kwa Ukraine na raia wake. Heshima hii pia ni kwako binafsi kwamba tumefurahi kuweza kuishughulikia, kwa sababu ujasiri wako, uwazi wako na kujitolea kwako ni vya kuvutia. alisema Macron.

Naye kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, alisisitiza matamshi ya Macron.

Tumejitolea pamoja na Ukraine, na pia tumeisaidia Ukraine kupitia misaada ya kifedha, misaada ya kibinadamu na silaha, silaha nzito nzito, mfumo wa ulinzi na hivi karibuni, utoaji wa vifaru vya kivita, na tutaendelea kufanya hivyo kwa muda mrefu iwezekanavyo.

 Zelensky aliwasili Paris kutoka London, ambako alikutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, Mfalme Charles III mapema jana Jumatano na kuzungumza na bunge, katika ziara yake ya pili nje ya nchi tangu kuanza kwa vita, karibu mwaka mmoja uliopita, baada ya ziara ya Washington mwezi Desemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.