Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Katika Bunge la Ulaya, Zelensky aonyesha kwamba mustakabali wa Ulaya unahusishwa na ule wa Ukraine

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amepongezwa na kupigiwa makofi na wabunge wa Ulaya huko Brussels Alhamisi, Februari 9, akiwa amesimama mbele la Bunge, wakati wa ziara iliyoelezwa kuwa ya "kihistoria" na Rais wa Bunge la Ulaya, Roberta Metsola. Volodymyr Zelensky, katika hotuba yake, ametaka kuwaonyesha waunge wa Ulaya ni kiasi gani mustakabali wa Ulaya unahusishwa na ule wa Ukraine.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky pamoja na Rais wa Bunge la Ulaya Roberta Metsola mnamo Februari 9, 2023 huko Brussels.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky pamoja na Rais wa Bunge la Ulaya Roberta Metsola mnamo Februari 9, 2023 huko Brussels. © Alain Rolland/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Baada ya hatua ya kwanza ya ziara yake huko London na Paris siku moja kabla, kiongozi wa Ukraine anashiriki Alhamisi hii huko Brussels katika mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi na serikali wa Umoja wa Ulaya, ambapo ataomba Kyiv kupewa ndege za kivita ili kukabiliana na kusonga mbele kwa jeshi la Urusi katika uwanja wa vita, karibu mwaka mmoja baada ya kuzuka kwa uvamizi wa Moscow.

Tangu mwanzo wa hotuba yake, Rais wa Ukraine amewashukuru wabunge na nchi wanachama kwa msaada wao usio na kikomo tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine, "njia pekee ya kusonga mbele," amesema. Pia amesisitiza juu ya 'nyumba hii ya Ulaya' ambayo ni mali ya raia wa Ukraine na wanataka kuwa wanachama. Bila shaka hii ni njia ya kukumbuka maombi ya Ukraine ya uanachama wa Umoja wa Ulaya. "Ombi hili ambalo lilitoa ujasiri na nguvu kwa Waukraine kusimama na kupigana. Ushindi dhidi ya Urusi utahakikisha udumishaji wa maadili ya Ulaya,” Volodymyr Zelensky amesema mbele ya wabunge wa Ulaya.

Rais Ukraine ameomba kwa nguvu kubwa na imani kwa wabunge hawa kuendelea na msaada wao. "Ni suala la maisha, kifo na Ulaya," amesema mwishoni mwa hotuba yake.

'Tupo pamoja nanyi muda wowote'

Roberta Metsola amesema katika hotuba yake, iliyokaribishwa na wabunge: "Sasa nchi lazima zizingatie, haraka, kama hatua inayofuata, kutoa mifumo ya masafa marefu na ndege ambavyo mnahitaji ili kulinda uhuru ambao watu wengi waliuchukulia kawaida... Jibu letu lazima liwe sawia na tishio, na tishio ni lipo... Tuko pamoja na tutazidi kuwa pamoja. "

"Ukraine ni Ulaya, mustakabali wa taifa lenu uko katika Umoja wa Ulaya. Tunajua dhabihu ambayo watu wako wamevumilia kwa Ulaya, na lazima tuiheshimu sio kwa maneno tu, bali pia kwa vitendo," amesisitiza. Nchi Ishirini na Saba wanachama wa Umoja wa Ulaya zimeipa Kyiv hadhi ya mgombea wa uanachama wa EU.

Katika tamko la pamoja, marais wa makundi mbalimbali ya kisiasa katika Bunge la Ulaya wametoa wito kwa nchi Ishirini na Saba wanachama wa Umoja wa Ulaya "kuongeza na kuharakisha usaidizi wao wa kijeshi, kutoa vifaa muhimu vya kijeshi na mifumo ya ulinzi na kutoa mafunzo kwa vikosi vya Ukraine".

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.