Pata taarifa kuu

Vifaru chapa Leopard kuwasili Ukraine hivi karibuni

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amesema washirika wake wanaweza kuanza kutuma magari ya kivita aina ya Leopard nchini Ukraine kuisaidia kupambana na Urusi, wakati huu Poland ikisema tayari imeomba idhini hiyo.

Kifaru chapa Leopard , hapa ilikuwa Finland Magharibi, Mei 4, 2022.
Kifaru chapa Leopard , hapa ilikuwa Finland Magharibi, Mei 4, 2022. AP - Heikki Saukkomaa
Matangazo ya kibiashara

Waziri mpya wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amesema kuwa anatarajia uamuzi wa haraka juu ya upelekaji wa vifaru vya kivita aina ya Leopard nchini Ukraine.

"Masuala ya kama vile ya matengenezo, ukarabati na upelekaji upya wa zana za kivita yanachunguzwa kabla ya kupelekewa vifaru hivyo" Pistorius amesema katika mkutano na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg mjini Berlin.

Pistorius amezihimiza nchi washirika ambazo zina vifaru chapa Leopard vinavyofanya kazi tayari kuanza kuwapa mafunzo wanajeshi wa Ukraine ya jinsi ya kuvitumia

Katibu Mkuu wa Jeshi la nchi za Mataifa Magharibi NATO, Jens Stoltenberg naye amesema magari hayo ya kivita yaliyotengezwa nchini Ujerumani, yataanza kuwasili Ukraine hivi karibuni. 

Ukraine imekuwa ikitoa wito kwa Ujerumani kutoa msaada wa magari na silaha zake, ili kuisaidia katika mapamabano dhidi ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.