Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE- MAPIGANO

Ujerumani imesema washirika wake wanaweza kuanza kutuma vifaru Ukraine

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amesema washirika wake wanaweza kuanza kutuma magari ya kivita aina ya Leopard nchini Ukraine kuisaidia kupambana na Urusi, wakati huu Poland ikisema tayari imeomba idhini hiyo.

Katibu Mkuu wa Jeshi la nchi za Mataifa Magharibi NATO, Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa Jeshi la nchi za Mataifa Magharibi NATO, Jens Stoltenberg AP - Alexandru Dobre
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Jeshi la nchi za Mataifa Magharibi NATO, Jens Stoltenberg naye amesema magari hayo ya kivita yaliyotengezwa nchini Ujerumani, yataanza kuwasili Ukraine hivi karibuni.

“Nilikuwa na mazungumzo mazuri leo kuhusu swala la Ujerumani  na nina matumaini kwamba  hivi karibuni patapatikana suluhu.”amesema Jens Stoltenberg.

Ukraine imekuwa ikitoa wito kwa Ujerumani kutoa msaada wa magari na silaha zake, ili kuisaidia katika mapamabano dhidi ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.