Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uturuki: uchaguzi wa rais utafanyika Mei 14, atangaza Erdogan

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan ametangaza Jumapili kwamba uchaguzi wa urais na wa wabunge utafanyika tarehe 14 Mei, 2023. 

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan. © Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

"Nitatumia mamlaka yangu kuendeleza uchaguzi hadi Mei 14," amesema Mkuu wa nchi wakati wa mkutano na vijana huko Busa (magharibi), akibainisha kuwa "si suala la 'uchaguzi wa mapema (...) lakini marekebisho ya kuzingatia (tarehe) ya mitihani'.

Uamuzi huo, uliojaa maana kwa uchaguzi unaofikiriwa kuwa mgumu zaidi katika miongo ya hivi karibuni, mara moja ulizua maswali mengi ya kisheria na kuibua mijadala mikali kati ya wataalamu na wawakilishi wa kisiasa wa kila aina.

Mkuu wa Nchi, mgombea wa katika kiti cha urais, alikua Waziri Mkuu mnamo 2003, kabla ya kurekebisha Katiba na kuwa rais, aliyechaguliwa moja kwa moja na kura ya maoni ya wote, mnamo 2014. Akiwa na umri wa miaka 68, Bw. Erdogan hivyo anawania kwa mara ya tatu katika uchaguzi wa urais. katika muktadha wa mzozo mkubwa wa kiuchumi na mvutano mkubwa wa kisiasa, ambapo ubabe wake na uhafidhina wake unapingwa na makundi mengi ya mashirika ya kiraia ya Kituruki. Kwa mara ya kwanza baada ya miaka ishirini, yeye sio kipenzi kisichopingika tena katika kura za maoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.