Pata taarifa kuu

Uturuki yafuta ziara ya waziri wa Uswisi baada ya maandamano dhidi ya Ankara kuruhusiwa

Uturuki imetangaza Jumamosi Januari 21 kwamba imefuta ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Uswisi, baada ya idhini iliyotolewa ya kufanya maandamano dhidi ya Uturuki huko Stockholm.

Waziri wa Ulinzi wa Uswisi Pal Jonson akizungumza na wanahabari wakati wanajeshi kutoka Ukraine wakishiriki katika mazoezi yaliyoandaliwa na wanajeshi wa pamoja wa kikosi cha usafiri (JEF), kaskazini mashariki mwa Uingereza mnamo Novemba 9, 2022.
Waziri wa Ulinzi wa Uswisi Pal Jonson akizungumza na wanahabari wakati wanajeshi kutoka Ukraine wakishiriki katika mazoezi yaliyoandaliwa na wanajeshi wa pamoja wa kikosi cha usafiri (JEF), kaskazini mashariki mwa Uingereza mnamo Novemba 9, 2022. AFP - ANDY COMMINS
Matangazo ya kibiashara

"Ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Uswisi Pål Jonson nchini Uturuki mnamo Januari 27 imepoteza umuhimu na maana yake, kwa hivyo tumefuta ziara hiyo," Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar amesema. Lengo la ziara hii lilikuwa ni kujaribu kuondoa pingamizi la Ankara kwa Uswisi kuingia NATO.

Idhini aliyopewa Rasmus Paludan, raia wa Uswisi mwenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia kuandamana Jumamosi saa sita mchana mbele ya ubalozi wa Uturuki katika mji mkuu wa Uswisi, imeikasirisha Ankara. Rasmus Paludan ameonyesha nia yake ya "kuchoma Quran" mbele ya washiriki. Maandamano, yanayounga mkono Uturuki wakati huu, yanapangwa wakati huo huo karibu na ubalozi.

Kesi hiyo mara moja iliamsha hasira ya Ankara. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlüt Cavusoglu amelaumu kuridhika kwa mamlaka ya Uswisi katika Twitter. Msemaji wa rais wa Uturuki Ibrahim Kalin ameshutumu maandamano hayo yaliyopangwa na kuyataja kuwa "uhalifu wa wazi wa chuki". "Kuruhusu hatua hii licha ya maonyo yetu yote ni kuhimiza uhalifu wa chuki na Uislamu," ameandika kwenye Twitter.

Uamuzi wa pamoja

Waziri wa Ulinzi wa Uswisi kwa upande wake amesema kuwa uamuzi wa "kuahirisha" ziara yake nchini Uturuki umechukuliwa pamoja na mwenzake wa Uturuki siku ya Ijumaa wakati wa mkutano kuhusu Ukraine huko Ramstein, Ujerumani. "Mahusiano na Uturuki ni muhimu sana kwa Uswisi na tunatazamia kuendelea na mazungumzo," Pål Jonson alitweet.

Siku ya Ijumaa, Uturuki ilimwita balozi wa Uswisi mjini Ankara "kulaani kitendo hiki cha uchochezi ambacho kinaashiria uhalifu wa chuki, kwa maneno makali zaidi", kulingana na chanzo cha kidiplomasia.

Ilikuwa ni mara ya pili katika siku chache kwamba mwakilishi wa Uswisi huko Ankara aliitwa na Wizara ya Mambo ya Nje, baada ya kutolewa wiki iliyopita kwa video inayoonyesha mnenguaji aliyenyongwa, iliyotambuliwa kama Rais Recep Tayyip Erdogan. Tamasha hili lilifanywa na kikundi kilicho karibu na Kamati ya Rojava, inayounga mkono Wakurdi wa Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.