Pata taarifa kuu

Uturuki: Wengi wajeruhiwa na bomu dhidi ya gari la polisi Diyarbakir

Watu tisa wakiwemo maafisa wanane wa polisi wamejeruhiwa Ijumaa hii, Desemba 16 nchini Uturuki katika mlipuko wa bomu baada ya gari la polisi kupita karibu na mji wa Diyarbakir, mji mkuu wa kusini-mashariki wenye Wakurdi wengi.

Maafisa wa polisi wakifanya ukaguzi wa usalama kwenye barabara ya Silvan, karibu na mjin wa Dyarbakir.
Maafisa wa polisi wakifanya ukaguzi wa usalama kwenye barabara ya Silvan, karibu na mjin wa Dyarbakir. REUTERS/Sertac Kayar
Matangazo ya kibiashara

Watu watano waliwekwa chini ya ulinzi. Shambulio hilo halijadaiwa na kundi lolote, lakini mamlaka inawashuku wapiganaji wa Kikurdi, ambao jeshi la Uturuki linakabiliana nao nchini Iraq na Syria.

Bomu hilo lilikuwa limefichwa kwenye gari lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara. Kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani, vilipuzi vililipuliwa kwa mbali, wakati gari la polisi lilipopita. Ilikuwa saa 11:10 alfajiri na bado kulikuwa na giza kwenye barabara hii inayounganisha mji wa Diyarbakir hadi Mardin, mji ulioko takriban kilomita ishirini kutoka mpaka wa Syria.

Wakurdi wanahusika?

Shambulio hilo halikusababisha majeraha makubwa, lakini liliamsha hisia kwa sababu lilikuwa la kwanza katika miaka mitano karibu na mji wa Diyarbakir. Shambulio hili Inakuja katika hali ya wasiwasi hasa kati ya Uturuki na wapiganaji wa Kikurdi ambao Waziri wa Mambo ya Ndani, Süleyman Soylu, aliwataja haraka kuwa wahusika wakuu. Kulingana na waziri huyo, mmoja wa waliokamatwa alikiri kuegesha gari lililokuwa limetegwa bomu.

Shambulizi hilo limetokea baada ya mashambulizi kadhaa ya angani ya jeshi la Uturuki dhidi ya kundi la PKK kaskazini mwa Iraq na dhidi ya kundi lao la Syria la YPG. Rais Erdogan alitishia katika wiki za hivi karibuni kufanya operesheni mpya ya kijeshi ya ardhini kaskazini mwa Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.