Pata taarifa kuu

Uturuki: Mlipuko mbaya katikati mwa Istanbul

Hofu imetanda kwa wakazi wa mji mkuu wa Uturuki, Istanbul, siku ya Jumapili baada ya mlipuko mkali usiojulikana asili yake na kusababisha vifo vya watu sita na wengine kadhaa kujeruhiwa kulingana na raiw wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdpogan ambaye amelaani kitendo hicho na kukiita 'shambulio baya'.

Waokoaji wawasili kwenye eneo la mlipuko katika mtaa wa Istiklal huko Istanbul mnamo Novemba 13, 2022.
Waokoaji wawasili kwenye eneo la mlipuko katika mtaa wa Istiklal huko Istanbul mnamo Novemba 13, 2022. AP - Francisco Seco
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo ulitokea mwendo wa saa 10:20 alaasiri saa nchini Uturuki, wakati umati mkubwa wa watu wamekuwa wamekusanyika katika eneo hili maarufu linalotembelewa na watu wengi siku za Jumapili kwa wakazi wa Istanbuli na watalii. Chini ya saa moja baada ya tukio hilo baya, Baraza Kuu linalosimamia vyombo vya habari nchini Uturuki (RTUK) limepiga marufuku vyombo vya habari kurusha picha za tukio hilo.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aelaani "shambulio baya" ambalo limesababisha "vifo vya watu sita na 58 kujeruhiwa", kulingana na ripoti ya hivi punde Jumapili huko Istanbul, amesema moja kwa moja kwenye televisheni. "Wahusika wa shambulio hili baya watajulikana. Raia wetu wawe na uhakika kwamba wahalifu wataadhibiwa,” amesema, saa mbili baada ya mlipuko katika barabara ya kibiashara ya Istiklal.

"Ushuhuda wa kwanza unaonyesha kuwa lilikuwa shambulio la kigaidi", amebainisha rais, mbele ya waandishi wa habari, na kuongeza kuwa "mwanamke mmoja amehusika katika shambulio hili", bila maelezo zaidi. Uvumi ulienea mara baada ya mlipuko huo, kuhusu shambulio la kujitoa mhanga, bila uthibitisho wowote au ushahidi.

"Wahusika wa shambulio hili baya watafichuliwa. Watu wetu wawe na uhakika kwamba wahusika wataadhibiwa,” aliahidi saa mbili baada ya mlipuko huo. "Jaribio la kuinasa Uturuki na taifa la Uturuki kwa chochea hofu haziwezi kufikia lengo lake leo au kesho, kama vile walivyofanya jana," rais ameongeza.

"Nilikuwa umbali wa mita 50-55, ghafla ukasikika mlio wa mlipuko. Niliona watu watatu au wanne chini,” shahidi, Cemal Denizci, 57, ameliambia shirika la habari la AFP. "Watu walikuwa wakikimbia kwa hofu. Kelele zilikuwa kubwa. Kulikuwa na moshi mweusi. Mlio ulikuwa mkubwa,” ameongeza. Watu wameondolewa katika eneo la tukio.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.