Pata taarifa kuu

Recep Tayyip Erdogan azituhumu nchi za Magharibi kwa kuichokoza Urusi

Akisafiri kuelekea Belgrade siku ya Jumatano kukutana na mwenzake wa Serbia, Recep Tayyip Erdogan alishutumu nchi za Magharibi kwa "uchokozi" dhidi ya Urusi. Siku moja kabla, rais wa  Uturuki alizilaumunchi za Magharibi na vikwazo vyao dhidi ya Moscow kufuatia mgogoro wa nishati.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa Serbia Aleksandar Vucic mjini Belgrade Septemba 7, 2022.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa Serbia Aleksandar Vucic mjini Belgrade Septemba 7, 2022. AP - Darko Vojinovic
Matangazo ya kibiashara

Recep Tayyip Erdogan amekanusha madai kwa wale waliotabiri miezi sita iliyopita kuwa vita vya Ukraine vitaileta Uturuki na nchi za Magharibi karibu zaidi.  Raiswa Uturuki hajabadilisha matamshi yake, ambayo kwa miaka mingi yamejumuisha kuzilaumu nchi za Magharibi kwa machafuko katika eneo hilo.

Amebaini, dhidi ya Urusi, “nchi za Magharibi zinafuata sera yenye msingi wa uchochezi. Humuweza kupata suluhu kwa njia hiyo,” alisema.

Recep Tayyip Erdogan anapingana na nchi za Magharibi sera yake inayoitwa "usawa" kati ya Kyiv na Moscow, ambayo ilimuwezesha, msimu huu wa joto, kujadili makubaliano ya kuanza tena usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine. Kwa nguvu ya mafanikio haya ya kidiplomasia, rais wa Uturuki anajitokeza kama mkosoaji, akienda mbali na kuchukua baadhi ya hoja kutoka Urusi.

"Urusi sio nchi ambayo inaweza kuchukuliwa kirahisi. Urusi imepunguza usambazaji wa gesi, bei imeongezeka ghafla barani Ulaya, na sasa kila mtu anashangaa jinsi watakavyopitia msimu wa baridi, rais wa Uturuki alisema. Ni dhahiri kwamba kila mtu akiishambulia, Urusi itatumia njia, silaha iliyo nayo. »

Uturuki, ikiwa na hamu ya kuhifadhi jukumu lake kama mpatanishi na uhusiano wake wa kiuchumi na Urusi, inakataa Urusi kuwekewa vikwazo. Hii haiizuii kuisaidia Ukraine kijeshi, kwa kuipatia ndege zisizo na rubani na magari ya kivita. Katika taarifa hiyo, Recep Tayyip Erdogan pia alishutumu nchi za Magharibi kwa kujifanya kutuma silaha kwa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.