Pata taarifa kuu

Chama cha Kurdistan's Workers' Party (PKK) chahusihwa na shambulio baya Istanbul

Waziri wa Mambo ya ndani wa Uturuki, Suleyman Soylu amekishtumu chama cha Kurdistan's Workers' Party (PKK) kwa kuhusika na shambulio la bomu jijini Istanbul na kusababisha vifo vya watu sita na kuwajeruhi wengine zaidi ya 80. 

Waziri wa Mambo ya ndani wa Uturuki, Suleyman Soylu.
Waziri wa Mambo ya ndani wa Uturuki, Suleyman Soylu. Ahmet Bolat/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Pamoja na shutuma hizi, Waziri huyo amesema mmoja wa watu waliohusika na shambulio anayeaminiwa kutega bomu himo, amekamatwa. 

Shambulio hilo lilitokea katika barabara yenye shughuli nyingi ya Istiklal hapo jana. 

Uturuki, imeiorodhesha chama cha PKK kama shirika la kigaidi linaloungwa mkono na mataifa ya nje. 

Rais Recep Tayyip Erdogan naye pia amelaani shambulio hilo alilosema dalili zote zimeonesha kuwa ni kla kigaidi. 

Mwaka 2015, shambulio lingine lilitokea katika barabara hiyo ya    Istiklal wakati wa kampeni za kisiasa, na nchi hiyo imekuwa ikishuhudia matukio lama haya ambayo yamehusishwa na kundi la Islamic State. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.