Pata taarifa kuu

Umoja wa Ulaya wakubaliana kuhusu bei kikomo ya gesi

Nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya zimefikia makubaliano kuhusu kikomo cha bei ya gesi asilia, Jumatatu, Desemba 19, 2022. Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya Jumatatu zimeidhinisha utaratibu wa kupunguza bei ya jumla ya gesi kutoka euro 180/MWh.

Bei ya gesi itapunguzwa kutoka euro 180/MWh katika Umoja wa Ulaya, kulingana na makubaliano yaliyoafikiwa na nchi Ishirini na Saba wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Bei ya gesi itapunguzwa kutoka euro 180/MWh katika Umoja wa Ulaya, kulingana na makubaliano yaliyoafikiwa na nchi Ishirini na Saba wanachama wa Umoja wa Ulaya. AFP - ERIC PIERMONT
Matangazo ya kibiashara

Utaratibu wa kuweka kikomo, uliowekwa baada ya wiki kadhaa za majadiliano magumu, utaamilishwa tu kwa kiwango cha bei ya juu ya wastani wa bei ya kimataifa ya gesi ya kimiminika (LNG) ili kutohatarisha usambazaji wa gesi wa Ulaya, chanzo cha kidiplomasia kimesema.

Mawaziri wa Nishati wa Ulaya, waliokutana mjini Brussels, "wamefikia makubaliano muhimu ambayo yatalinda wananchi kutokana na kupanda kwa bei ya nishati, kwa utaratibu halisi na ufanisi, unaojumuisha dhamana muhimu kwa usalama wa usambazaji na utulivu wa masoko ya fedha," amesema Waziri wa Jamhuri ya Czech, Jozef Sikela, ambaye nchi yake inashikilia urais wa Umoja wa Ulaya, EU.

Mawaziri wa nchi Ishirini na Saba wanachama wa Umoja wa Ulaya walikuwa tayari wamekubaliana mnamo Desemba 13 juu ya baadhi ya masharti ya utaratibu, ambayo yatatumika kwa mikataba ya baadaye kwenye masoko ya gesi, lakini bado walipaswa kukubaliana juu ya bei ambayo kikomo kitahusika.

Hapo awali Tume ya Ulaya ilikuwa imependekeza kukomesha kandarasi za kila mwezi kwenye soko la marejeleo la TTF mara tu zitakapozidi euro 275/MWh kwa wiki mbili mfululizo, miongoni mwa masharti mengine - mambo ambayo hayajawahi kufikiwa, hata katika kilele cha kupanda kwa bei mwezi Agosti. TTF, jukwaa la Uholanzi, ni ubadilishanaji wa gesi halisi wa Umoja waUlaya, EU, na bei yake hutumika kama kigezo cha shughuli nyingi za gesi katika bara hilo.

Mpango mgumu kupatikana

Baada ya kutengana kuhusu pendekezo hili, nchi Wanachama hatimaye zimekubaliana juu ya kizingiti cha chini zaidi, ambacho kitatakiwa kufikiwa katika kipindi kilichopunguzwa kwa kiasi kikubwa. Mkataba wa utoaji katika mwezi mmoja umekuwa ukiuzwa Jumatatu kwenye TTF karibu euro 110/MWh.

Mataifa kadhaa (Uhispania, Poland, Ugiriki, Italia, n.k.) yalikuwa yametoa wito wa kulegezwa wazi kwa masharti ya kuwezesha utaratibu huo. Kinyume chake, kwa kusitasita kuingilia kati, mataifa mengine (Ujerumani, Uholanzi, Austria, nk.) yalidai "ulinzi" mkali ili kuzuia kikomo kutishia usamazaji wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.