Pata taarifa kuu

Qatar yatangaza kandarasi kuu ya gesi kuisambaza Ujerumani

Qatar imetangaza Jumanne wiki hii makubaliano makubwa ya kuipatia Ujerumani gesi asilia ya kimiminika, Liquefied Natural Gas(LNG) kwa miaka 15, katikati ya mzozo wa nishati duniani uliosababishwa na vita nchini Ukraine.

Waziri wa Nishati wa Qatar, Saad Sherida Al-Kaabi.
Waziri wa Nishati wa Qatar, Saad Sherida Al-Kaabi. KARIM JAAFAR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Β 

Makubaliano haya, yaliyohitimishwa kati ya Qatar Energy na kampuni ya Kimarekani ya ConocoPhillips, yatachangia "juhudi zinazolenga kusaidia usalama wa nishati nchini Ujerumani na Ulaya", amesema Waziri wa Nishati wa Qatar, Saad Sherida Al-Kaabi, wakati wa hafla ya kutia saini huko Doha.

Chini ya masharti ya mkataba huu, nchi ya Ghuba itatoa kuanzia mwaka wa 2026 "hadi tani milioni 2 za LNG kwa mwaka" kwa kituo cha gesi kinachoendelea kujengwa huko Brunsbutell, kaskazini mwa Ujerumani, amesema waziri wa Nishati.

Uwasilishaji utatolewa kwa "angalau miaka 15" na ConocoPhillips, mshirika wa Qatar Energy katika maendeleo ya uwanja wa pwani ya Kaskazini, kisima kikubwa zaidi cha gesi asilia ulimwenguni, ambacho Qatar inachangia na Iran.

Mkataba huu ni "mchango muhimu kwa usalama wa nishati duniani", amesisitiza Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Marekani, Ryan Lance.

Nchi za Ulaya zimekuwa zikitafuta mbadala wa gesi ya Urusi tangu Urusi ilipovamia Ukraine mnamo mwezi Februari mwaka jana.

Lakini mazungumzo na Qatar yamekuwa magumu, kwani Ujerumani na nchi nyingine zimekataa kutia saini mikataba ya muda mrefu sawa na ile inayounganisha nchi hiyo ya Ghuba na wateja wake wakuu barani Asia.

Wiki iliyopita, Qatar ilifikia rekodi ya mkataba wa miaka 27 na China, wa tani milioni 4 kwa mwaka.

Maafisa wa Qatar hawakushughulikia suala la bei, lakini muda mfupi na tarehe za mwisho za mkataba na Ujerumani zinapaswa kuhusishwa na malipo, wataalamu wa soko wanabaini.

- Mazungumzo makali -

Saad Sherida Al-Kaabi amesema kuwa Qatar Energy ilikuwa katika mazungumzo na makampuni ya Ujerumani ili kuongeza "kiasi" kinachotolewa na nchi yake.

Gesi ambayo itawasilishwa kwa Ujerumani kuanzia mwaka 2026 itatoka maeneo ya Kaskazini ya Kusini na Kaskazini ya Mashariki, itakayotengenezwa na makampuni makubwa ya nishati ya Magharibi, ikiwa ni pamoja na TotalEnergies ya Ufaransa na Shell ya Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.