Pata taarifa kuu

Shambulio dhidi ya kituo cha umeme cha Zaporizhia: IAEA yatoa wito 'kukomesha uhasama'

Wasiwasi unaendelea nchini Ukraine, Jumatatu hii, Novemba 21, baada ya shambulio jipya dhidi ya kito cha umeme cha Zaporizhia. Mkuu wa shirika la kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), akiwa na wasiwasi mkubwa, anatoa wito wa "kusitishwa mara moja kwa wazimu huu " kwa hofu bila shaka kwamba shambulio hili litaishia kusababisha maafa makubwa.

Rafael Grossi (picha yetu), Mkuu wa IAEA, amethibitisha hilo: "Kulikuwa na uharibifu katika sehemu nyeti" za kituo cha umeme cha Zaporizhia.
Rafael Grossi (picha yetu), Mkuu wa IAEA, amethibitisha hilo: "Kulikuwa na uharibifu katika sehemu nyeti" za kituo cha umeme cha Zaporizhia. AP - Markus Schreiber
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hili jipya lilifanyika Jumapili Novemba 20; hata hivyo halikusababisha uharibifu mkubwa, lakini liliathiri mitambo muhimu.

Mkuu wa shirika la kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, amethibitisha hilo: "Kulikuwa na uharibifu katika sehemu nyeti", ametangaza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa BFMTV. "Vinu havikupigwa," amesema, lakini "eneo ambalo mafuta yalipo." Kwa wakati huu, viwango vya mionzi vinaendelea kuwa vya kawaida, lakini ukweli ni kwamba urushaji huu wa makombora kunaleta wasiwasi mkubwa: je, vita vya Ukraine vitasababisha maafa ya nyuklia na atahiri zisizoweza kuhesabiwa?

Tathmini

Kwa sasa, wakaguzi wawili wa IAEA waliopo kwenye kituo cha umeme cha Zaporizhia wanatathmini uharibifu. Kwa hiyo kutajulikana zaidi katika saa zijazo kuhusu kiwango cha uharibifu huo, pengine, pia kuhusu upande uliotekeleza shambulio hilo. Kwa sababu, kama kila wakati tangu kituo hiki kilengwe na milipuko ya mabomu, Urusi na Ukraine zinashutumiana kila mmoja kwa kuhusika na mashambulizi.

'Mashambulizi ya maksudi na yaliyopangwa'

IAEA, kwa sasa, inasema haiwezi kubainisha asili ya mashambulizi haya. Hata hivyo, Rafael Grossi ana wasiwasi: watu wanaofanya hivi wanajua wapi wanapiga, mashambulizi haya ni ya "makusudi na yamepangwa", amesema, akitoa wito wa "kusitisha wazimu huu". "Yeyote yule, hii lazima ikome mara moja," Mkuu wa shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.