Pata taarifa kuu

Ukraine: Meya wa Kyiv azuru Brussels kwa majadiliano juu ya ujenzi

Jumatatu hii, Novemba 28, Meya wa mji wa Kyiv, Vitali Klitschko, anatarajiwa katika mji mkuu wa Ulaya ambako atapokelewa na mwenzake, Meya wa Brussels, Philippe Close. Viongozi hao wawili watashiriki katika Jukwaa la saba la Uwekezaji la Kyiv. Mwaka huu jukwa hilo litaleta pamoja viongozi wa serikali, viongozi wa Ulaya na Ukraine na kikao hiki kinatarajiwa kuzingatia ujenzi wa mji mkuu wa Ukraine.

Meya wa mji wa Kyiv Vitali Klitschko akiwa ofisini kwake katika Halmashauri ya Jiji katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, Ijumaa, Novemba 18, 2022.
Meya wa mji wa Kyiv Vitali Klitschko akiwa ofisini kwake katika Halmashauri ya Jiji katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, Ijumaa, Novemba 18, 2022. AP - John Leicester
Matangazo ya kibiashara

Ondoa vifusi, jenga upya majengo, rekebisha miundombinu iliyoharibiwa na mmashambulizi makubwa ya Urusi. Kujitayarisha kwa kipindi cha baada ya vita ni changamoto kubwa sana ambayo Kyiv na eneo lake vinasubiri.

Na matarajio ya mamlaka katika mji mkuu wa Ukraine ni makubwa. Lakini pia watalazimika kusaidiwa kuanzisha huduma za kisasa zaidi za kidijitali na suluhu za kiteknolojia. Kwa hivyo maneno matatu muhimu yako kwenye ajenda ya majadiliano yanayofanyika Brussels siku ya Jumatatu: uthabiti, uvumbuzi na uendelevu.

Ili kutekeleza kazi hii ngumu, pesa nyingi pia zinahitajika. Wawakilishi wa sekta ya umma na kibinafsi watashiriki katika mazungumzo hayo. Wataungwa mkono na taasisi za kifedha za kimataifa na wawekezaji binafsi, pia waliopo katika mji mkuu wa Ulaya. "Tunapaswa kujiandaa kwa siku zijazo," Vitali Klitschko amesema kabla ya kuwasili katika mji mkuu wa Ubelgiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.