Pata taarifa kuu

Jens Stoltenberg: NATO haitoacha kuiunga mkono Ukraine na kuipa misaada isiyo hatari

Katibu Mkuu wa Jeshi la nchi za Magharibi NATO, Jens Stoltenberg, amesema Ujerumani iko huru kuamua iwapo itaipa Ukraine mitambo ya kuzuia mashambulio ya angaa kutoka nchini Urusi baada ya Poland, kutoa wito kwa Berlin kutoa msaada huo kufuatia shambulio la hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya NATO, Ijumaa, Novemba 25, 2022 mjini Brussels, kabla ya Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa NATO unaofanyika Novemba 29 na 30 huko Bucharest, Romania.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya NATO, Ijumaa, Novemba 25, 2022 mjini Brussels, kabla ya Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa NATO unaofanyika Novemba 29 na 30 huko Bucharest, Romania. AP - Olivier Matthys
Matangazo ya kibiashara

Aidha, Stoltenberg amesema nchi wanachama wa NATO zitaendelea kuisaidia Ukraine. 

"Jumuiya ya Kujihami ya NATO haitoacha kuiunga mkono Ukraine na haitosita vile vile kuipa misaada isiyo hatari, " amesema Katibu Mkuu wa Jeshi la nchi za Magharibi NATO, Jens Stoltenberg. Akizungumza mjini Brussels leo kuelekea mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa jumuiya hiyo utakaofanyika huko Bucharest wiki ijayo, Stoltenberg amesema NATO itaendelea kusimama na Ukraine na haitorudi nyuma.

 Mashambulizi ya Urusi yamelaaniwa na marafiki wa Ukraine ila Urusi inasema inalenga tu miundo msingi inayohusishwa na jeshi. Urusi inasema Ukraine inaweza kusitisha mateso wanayopitia raia wake iwapo tu itayakubali matakwa yake.

Katika hatua nyingine, rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, ameyataka mataifa ya Ulaya kusimama pamoja dhidi ya Urusi, huku rais Vladimir Putin akikutana na akima mama ambao watoto wao wanapigana nchini Ukraine na kuwaamnbia kuwa wawe makini na taaryfa za uongozi zinazosambazwa kwenye mitandao kuhusu vita hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.