Pata taarifa kuu

Italia: Waziri Mkuu mteule, Giorgia Meloni atangaza serikali yake

Waziri Mkuu mpya Giorgia Meloni na mawaziri wake, ambao wameunda serikali inayoegemea siasa za mrengo mkali wa kulia tangu 1946, wameapishwa Jumamosi (Oktoba 22) katika ikulu ya rais ya Quirinal huko Roma.

Rais wa Italia Sergio Mattarella na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni wakati wa hafla ya kuapishwa katika Ikulu ya Quirinal mjini Roma, Jumamosi Oktoba 22, 2022.
Rais wa Italia Sergio Mattarella na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni wakati wa hafla ya kuapishwa katika Ikulu ya Quirinal mjini Roma, Jumamosi Oktoba 22, 2022. AP - Alessandra Tarantino
Matangazo ya kibiashara

Sherehe hiyo katika ikulu ya rais ya Quirinal, makazi ya Papa na Wafalme wa Italia kabla ya kuwa ikulu ya rais wa Jamhuri, imefanyika asubuhi, Jumamosi, mbele ya rais wa nchi hiyo Sergio Mattarella.

Siku ya Ijumaa, Giorgia Meloni, 45, alikuwa amekubali jukumu la Rais wa Baraza la Italia, na hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kuitwa kushikilia wadhifa huu katika historia ya nchi. Kisha akawasilisha muundo wa serikali yake.

Akiwa amevalia suti nyeusi, Giogia Meloni alikuwa wa kwanza kula kiapo, akifuatiwa na Manaibu Mawaziri wakuu wake wawili kutoka vyama viwili washirika katika muungano wake, Matteo Salvini, kiongozi wa shirika linalopinga Wahamiaji, na Antonio Tajani, afisa mkuu wa chama cha Silvio Berlusconi cha Forza Italia.

Baada ya kuidhinishwa kwa wingi wa kura katika Bunge, serikali hii mpya itaanza kazi mwanzoni mwa wiki ijayo.

"Ujumbe unaojumuisha viongozi wa vyama na waku wa taasisi zote za kisiasa za muungano wa mrengo wa kulia uliokutana na Rais Mattarella ulikubaliana na Rais Mattarella juu ya haja ya kulipatia taifa hili serikali mpya haraka iwezekanavyo, kwa sababu dharura zinatukabili ni nyingi mno kitaifa na kimataifa. Muungano mzima ambao, bila ya kustaajabisha, ulikutana kwa mashauriano, ulitoa dalili kwa kauli moja, tuseme, sawa na wingi wa wabunge, kwa kupendekeza kwa Rais wa Jamhuri kwamba aniteue mimi kuwa mtu mwenye dhamana ya kuunda serikali mpya, " amesema Giorgia Meloni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.