Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Italia: Muungano wa mrengo wa kulia washinda viti vingi, Meloni adai uongozi wa serikali

Nchini Italia, mrengo wa kulia unaoongozwa na Giorgia Meloni wa chama cha Brothers of Italy,  umeonekana kupata wingi wa kura katika uchaguzi uliofanyika jana , hali ambayo huenda ikamfanya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa waziri mkuu nchini humo.

Giorgia Meloni kwenye jukwaa kwenye makao makuu ya chama chake,Brothers of Italy, mjini Roma, Septemba 26, 2022.
Giorgia Meloni kwenye jukwaa kwenye makao makuu ya chama chake,Brothers of Italy, mjini Roma, Septemba 26, 2022. REUTERS - GUGLIELMO MANGIAPANE
Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya awali kwa mujibu wa  shirika la utangazaji la serikali la RAI, yanaonesha kuwavyama vya kihafidhina, ambavyo pia vinajumuisha chama cha wanasiasa Matteo Salvini na kile cha Silvio Berlusconi, vilishinda kati ya asilimia 41 na 45, kutosha kuhakikisha udhibiti wa mabunge yote mawili.

Iwapo matokeo haya yanayotarajiwa hivi leo yataidhinishwa, chama chake Meloni kitakuwa kimepiga hatua kubwa, baada ya uchaguzi wa mwaka 2018 kilipata asilimia 4 pekee ya kura,  lakini wakati huu, kimepata matokeo mazuri.

Uchaguzi huu wa kwanza wa kitaifa nchini humo katika zaidi ya karne moja, ulichochewa na mizozo ya vyama ambayo iliiangusha serikali ya umoja wa kitaifa ya Waziri Mkuu Mario Draghi mwezi Julai.

Italia ina historia ya kutokuwa na utulivu wa kisiasa na waziri mkuu ajaye ataongoza serikali ya 68 ya nchi hiyo tangu 1946 na kukabiliwa na changamoto nyingi, haswa kupanda kwa gharama za nishati na changamoto za  kiuchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.