Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Salvini azua gumzo kwa kupinga vikwazo dhidi ya Urusi

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Italia, Matteo Salvini amezua gumzo kwa kuhoji vikwazo dhidi ya Urusi tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Italia, Matteo Salvini.
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Italia, Matteo Salvini. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

"Putin hangeweza kusema vizuri zaidi". Mzozo huo unazidi kuongezeka nchini Italia Jumapili hii, Septemba 4, kufuatia matamshi ya Matteo Salvini ambaye alitilia shaka ufanisi wa vikwazo vya Umoja wa Ulaya vilivyochukuliwa dhidi ya Urusi ili kukomesha uvamizi wake nchini Ukraine.

"Miezi kadhaa imepita na watu wanalipa bili zao mara mbili au hata mara nne zaidi, na baada ya miezi saba vita vinaendelea na hazina ya Shirikisho la Urusi inajaa pesa," ameiambia redio ya RTL. "Tunahitaji ngao ya Ulaya" kulinda biashara na familia, kama wakati wa janga la UVIKO, Matteo Salvini amebaini kufuatia mjadala ulioandaliwa kama sehemu ya Jukwaa la Uchumi The European House - Ambrosetti huko Cernobbio, kaskazini mwa Italia.

"Ikiwa tunataka kuendelea na vikwazo, tufanye hivyo, tunataka kuilinda Ukraine, lakini nisingependa hilo badala ya kuwadhuru waliowekewa vikwazo, tujidhuru wenyewe," alisema. "Je, vikwazo vinafanya kazi? Hapana. Hadi leo, waliowekewa vikwazo ni washindi, huku waliotekeleza vikwazo hivyo wamesalimu amri,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter siku moja kabla.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.