Pata taarifa kuu

Elimu: Jinsi mgogoro wa Ukraine ulivyobadilisha shule nchini Urusi

Alhamisi, Septemba 1 ndio mwaka mpya wa shule ulioanza nchini Urusi chini ya ishara ya 'operesheni maalum': watoto wa shule wa maeneo yaliyotekwa na vikosi vya Urusi na washirika wake wanaounga mkono Urusi huko Donbass na kusini mwa Ukraine tapewa, kama Wanafunzi wa shule za Urusi, mitaala mipya, kwa msisitizo juu ya umuhimu wa kufundisha toleo la historia lililoidhinishwa na Kremlin, lakini pia kozi mpya za uzalendo shuleni

Rais wa Urusi Vladimir Putin akisalimiana na mwanafunzi mmoja baada ya hotuba yake ya kuanza kwa mwaka wa shule, Kaliningrad, Septemba 1, 2022.
Rais wa Urusi Vladimir Putin akisalimiana na mwanafunzi mmoja baada ya hotuba yake ya kuanza kwa mwaka wa shule, Kaliningrad, Septemba 1, 2022. via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Vladimir Putin alitoa hotuba ya kila mwaka shule zinapoanza mwaka wa masomo, kutoka Kaliningrad, siku ya Alhamisi. Kisha alikutana na watoto wa shule waliochaguliwa kote nchini kwa Maswali na Majibu ya saa moja. Rais wa Urusi alikariri kwamba alilazimika kutuma wanajeshi "kutetea wazungumzaji wa Kirusi wa mashariki mwa Ukraine". Lakini pia alisisitiza juu ya umuhimu wa kufundisha toleo la historia kama vile amekuwa akiitetea kila wakati:

Jana nilizungumza na Waziri wa Elimu Sergei Kravtsov. Alirudi kutoka Donetsk na maeneo mengine. Alichoniambia, samahani, lakini macho yangu hayaoni vizuri. Watoto wa shule hawajui hata kuwa Daraja la Crimea lilikuwepo. Ndio, hawajui, wanadhani ni habari za uwongo! Wala hawajui hata kama Ukraine na Urusi ni sehemu ya taifa moja. Ndivyo walivyofundishwa historia. Hata watu wazima pengine hawajui kwamba Ukraine kamwe hikuwa taifa huru kabla ya kuundwa kwa jamhuri ya Sovieti (USSR).

.Vyombo vya habari vya Urusi viliunga mkono hili. Vitabu vya shule kutoka kwa maeneo yaliyotekwa vimepangwa, na sio tu kwa sababu sasa ni muhimu kuzipa shule toleo lingine la historia ya Ukraine. Nina Ostanina, mbunge wa kikomunisti na mwenyekiti wa kamati ya masuala ya familia, wanawake na watoto, anaeleza:

Watoto wanapaswa kujua historia ya nchi yao. Tumeteseka, kwa kujutia, kwa miaka thelathini, kupotoshwa kwa historia na wazalendo wanaodai kuwa ni wa kiliberali, chini ya shinikizo la Jumuiya ya nchi za Magharibi, kwa kiasi kikubwa chini ya ushawishi wa miongozo ya Soro ambayo, chini ya kivuli cha hisani , zimesambazwa sana katika shule zetu na kwa watoto wetu. Upotoshaji huu wa historia umesababisha ukweli kwamba kizazi kizima hakina tena wazo lisilo kamili, lakini kwa kweli wazo potofu la jukumu la watu wa Sovieti katika malezi ya nchi yetu. Wengi, hata watu wetu wa Urusi, hawajui historia ya Vita Kuu ya Uzalendo

Na hatutaki watoto wetu wapate hatima sawa na vijana wa Ukraine, ambao wamesahau ninani wanadaiwa uhuru wao. Hatungetaka watoto na vijana wetu wapate hatima sawa na katika nchi za Baltic, ambapo makaburi ya kuheshimu askari wa Sovieti yanaangushwa na kubomolewa.

Uzalendo uliopo sasa hivi

Tangu Februari 24, Kremlin imekuwa ikishibikiza shule kuwa za kizalendo zaidi. Na tangu Alhamisi hii, Septemba 1, wanafunzi wote sasa wanaanza wiki kwa sherehe ya kuinua bendera na kuimba wimbo wa taifa. 

"Matukio kama haya yatasababisha migogoro bila shaka. Si kati ya walimu na utawala, au wanafunzi na utawala, lakini kati ya wazazi na utawala. Wazazi wana msimamo wao, na ikiwa hauendani na ule ambao sasa umekuzwa rasmi, itasababisha migongano mingi. Ninajua kuwa katika maeneo mengi ambayo miji mikubwa iko, wasimamizi wanafahamu shida hii na wanajaribu kupunguza athari na kupunguza idadi ya migogoro inayoweza kutokea", amesema mwalimu mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.