Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi nchini Austria: Alexander Van der Bellen kuendelea kushikilia madaraka

Zaidi ya Waaustria milioni sita wameitishwa kupiga kura Jumapili hii, Oktoba 9, kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais. Rais wa sasa, mwanamazingira Alexander Van der Bellen, ndiye anayepewa nafasizaidi ya kushinda uchaguzi huo dhidi ya washindani wake. Hali tofauti sana na ile ya uchaguzi wa urais, miaka sita iliyopita.

Rais wa Austria Alexander Van der Bellen akiwa mbele ya bango lake la kampeni mnamo Septemba 23, 2022.
Rais wa Austria Alexander Van der Bellen akiwa mbele ya bango lake la kampeni mnamo Septemba 23, 2022. REUTERS - Leonhard Foeger
Matangazo ya kibiashara

Mnamo 2016, ilichukua duru tatu za uchaguzi, ya pili ikiwa ilibatilishwa, kwa Alexander Van der Bellen kushinda uchaguzi wa rais dhidi ya mshindani wake wa mrengo wa kulia Norbert Hofer. Lakini Jumapili hii, rais mwanamazingira huenda akashinda uchaguzi katika duru ya kwanza, vyama vingi vya kimila havikuwasilisha wagombea dhidi yake.

Nikusema kwamba jukumu lake limekuwa muhimu zaidi ya miaka sita iliyopita. Wakati, katika kipindi hiki, Austria ilipata serikali sita tofauti na migogoro mingi ya kisiasa, Alexander Van der Bellen aliweza kuwahakikishia Waaustria. Kupitia hotuba zake zenye umoja, heshima yake ya kina kwa Katiba na kuimarisha kidemokrasia, aliweza, katika kipindi cha machafuko ya kisiasa, kudumisha imani kwa taasisi. Kutokana na hali hii, sasa ndiye mwanasiasa anayependwa zaidi nchini Austria.

Uchaguzi huu kwa hiyo ni tofauti sana na ule wa miaka sita iliyopita, vigingi na mashaka ni finyu, pengine ndiyo maana hauwavutii Waustria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.