Pata taarifa kuu
Sri Lanka

Sri lanka : Waziri mkuu akubali kujiuzulu

Nchini Sri Lanka Waziri Mkuu Ranil Wickremesinghe yuko tayari kujiuzulu, ili kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, baada ya waandamanaji waliokuwa na hasira, kuvamia makaazi ya rais jijini Colombo.

Waandamanaji walimzingira rais jijini Colombo, mji mkuu wa Sri Lanka, Julai 9, 2022.
Waandamanaji walimzingira rais jijini Colombo, mji mkuu wa Sri Lanka, Julai 9, 2022. AP - Thilina Kaluthotage
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya waandamanaji kuvamia makaazi ya rais, yalilazimu kiongozi wa nchi hiyo Gotabaya Rajapaksa, kutoroshwa kufuatia shinikizo za wananchi waliomtaka ajiuzulu.

Maelfu ya waandamanaji wameonekana katika makaazi ya rais, wakiwa kwenye vyumba mbalimbali na wengine wakiogelea katika êneo la makaazi hayo ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73.

Hakuna maafisa wa usalama walionekana wakati wa uvamizi wa makaazi hayo, baada ya awali kulemewa na idade kubwa ya waandamanaji waliovunja malango ya makaazi hayo.

Kabla ya hatua hii ya waandamanaji, kumekuwa na maandamaano kwa miezi kadhaa, kulalamikia hali ngumu ya kiuchumi iliyosababisha kupanda kwa gharama ya maisha, huku bei ya mafuta, chakula na dawa zikipanda.

Waandamanaji wanailamu família ya Rajapaksa kwa matatizo wanayowakumba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.