Pata taarifa kuu

Polisi nchini Sri Lanka kutumia nguvu kuzuia vurugu wakati wa maandamano.

Polisi nchini Sri Lanka, imepewa agizo la kutumia nguvu pamoja na kutumia risasi za moto kuzuia vurugu wakati huu  misururu ya maandamano ikiendelea  kushuhudiwa kwenye taifa hilo hata baada ya kujiuzulu kwa waziri mkuu Mahinda Rajapakse.

Polisi wakiwakabili waandamanji nchini Sri Lanka.
Polisi wakiwakabili waandamanji nchini Sri Lanka. AP - Eranga Jayawardena
Matangazo ya kibiashara

Raia nchini humo wamekuwa wakiaandamana kutaka serikali ya rais Gotabaya Rajapaksa kujiuzulu kutokana na hali mbaya ya uchumi inayolikumba taifa hilo mamlaka zikieleza kuwa kinachoedelea ni uhalifu wala sio maandamano ya kwaida.

Taarifa ya polisi inasema watu wanane wameripotiwa kufariki  nchini humo tangu  jumatatu wakati wafuasi wanaoiunga mkono serikali walipokabiliana na waandamanji wanaoipinga serikali ,makabiliano yaliosababisha pia  kujeruhiwa kwa watu 200 .

Agizo hilo linakuja wakati ambapo makataa ya watu kutembea nje nyakati za usiku yakiwa yametangazwa nchini humo ripoti zikisema kuwa hoteli ya kifahari inayomilikiwa na mtu wa karibu wa rais Rajapaksa ilichomwa moto siku ya jumanne jioni.

Waandamanji wameendelea kuonekana wakipiga kambi nje ya ofisi ya rais Rajapaksa licha ya kutangazwa kwa makataa ya watu kutembea usiku hali inayoendelea kutoa shinikizo zaidi kwa kiongozi huyo kujiuzulu.

Licha ya waziri mkuu kutangaza kujiuzulu raia wamekuwa wakitaka familia yote ya Rajapaksa kuondoka uwongozini wakituhumu familia hiyo  kwa kuhusika na ufisadi swala ambalo limetajwa  kuchangia pakubwa  katika matatizo yanayoikumba nchi hiyo.

Hali ngumu ya kiuchumi inayoshuhudiwa nchini Sri Lanka, imetajwa kuwa mbaya zaidi tangu nchi hiyo kupata uhuru wake mwaka wa 1948 bidhaa muhimu kama vile chakula, mafuta na dawa kwa miezi kadhaa sasa.

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis akiwa wa hivi punde kutoa wa kufanyika kwa mazungumzo ilikumaliza machafuko yanayoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.