Pata taarifa kuu

Budapest haitaki vikwazo zaidi dhidi ya Moscow

Umoja wa Ulaya unapaswa kusitisha mpango wake wa kuongeza vikwazo dhidi ya Urusi na kushinikiza kusitishwa kwa mapigano na kuweka mbele mazungumzo, mshauri wa Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban alisema siku ya Alhamisi.

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya huko Brussels mnamo Mei 30, 2022.
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya huko Brussels mnamo Mei 30, 2022. REUTERS - JOHANNA GERON
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kando ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya ambapo nchi Ishirini na Saba wa umoja huo walitoa rasmi hadhi ya Ukraine na Moldova kuwania kwenye nafi ya uanachama wa Umoja wa Ulaya, Balazs Orban alisema anaamini kuwa vikwazo vipya vitaiadhibu Umoja wa Ulaya zaidi ya Urusi.

Inategemea sana uagizaji wa hidrokaboni kutoka Urusi, Hungary inadhibiti kadiri inavyoweza mipango ambayo inaona ni chuki dhidi ya Moscow, hasa kwa vile Urusi inajenga kinu cha nyuklia kwenye ardhi ya Hungary.

Awali Balozi wa Ukraine katika Umoja wa Ulaya Vsevolod Chentsov alisema ridhaa ya Umoja wa Ulaya ni ishara kwa Moscow kwamba Ukraine, na nchi nyengine zilizokuwa umoja wa Kisovieti haziwezi kuwa chini ya himaya ya Urusi. 

Ni muhimu sana kwa jamii nzima ya Ukraine, hasa kwa jeshi maana wana sababu ya wazi kupigania nchi yao. Nimeshangaa na nimewaambia hata na marafiki zangu kuwa wanajeshi wetu wanapiga simu nyumba na kuuliza kuhusu hatma ya ombi lao la kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.