Pata taarifa kuu
URUSI

Urusi yazishtumu nchi za Ulaya kwa kumzuia Waziri wake wa Mambo ya nje Sergei Lavrov

Urusi imeyashtumu mataifa ya barra Ulaya kwa kuzuia ndege ya Waziri wake wa Mambo ya nje Sergei Lavrov kutumia angaa zake, akiwa njiani kwenda nchini Serbia.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi  Sergei Lavrov
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imeikera Urusi, na kuzilaumu nchi za Bulgaria, Macedonia Kaskazini na Montenegro kwa hatua hiyo, inasema inalenga kuizua Moscow kuendeleza sera yake ya kigeni.

Waziri Lavrov amesema kitendo kilichofanyika hakikuwahi kufikirika kuwa kinaweza kutokea.

Katika hatua nyingine rais Vladimir Putin ameonya kuwa vikosi vyake vitashambulia maeneo mapya nchini Ukraine, iwapo mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani watatuma makombora ya kisasa ili kuisaidia Kiev.

Onyo hili la Urusi linakuja wakati Uingereza nayo ikisema inatuma makombora yake ya kwanza ya masafa marefu nchini Ukraine, ili kuisaidia kuilinda dhidi ya mashambulio kutoka kwa Urusi.

Mapigano makali yameendelea katika jimbo la Luhansk, Mashariki mwa Ukraine huku uogozi wa mji wa Severodonetsk ukisema hali inaendelea kuwa mbaya, licha ya vikosi vya Urusi kuonekana kurudishwa nyuma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.