Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Vikosi vya Urusi vyaegesha kwenye lango la jiji la Sievierodonetsk

Katika siku ya 92 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Alhamisi Mei 26, jeshi la Urusi linatafuta kwa nguvu wote kuuteka mji wa Sievierodonetsk, mashariki mwa Ukraine ambapo Kyiv, ambayo inaebdelea na udhibiti mkubwa.

Vikosi vinavyounga mkono Urusi vikifyatua makombora kuelekea mji wa Sievierodonetsk, Mei 24, 2022.
Vikosi vinavyounga mkono Urusi vikifyatua makombora kuelekea mji wa Sievierodonetsk, Mei 24, 2022. REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa Kongamano la Kiuchumi la Davos siku ya Jumatano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kouleba aliishutumu NATO kwamba "haijafanya lolote" dhidi ya uvamizi wa nchi yake ulioanzishwa na Urusi, na alipendelea kupongeza "maamuzi ya mapinduzi" ya Umoja wa Ulaya. Pia aliomba silaha kubwa zaidi za kivita.

Mji wa viwanda wa Sievierodonetsk, magharibi mwa mkoa wa Luhansk, unakaribia kuzingirwa na jeshi la Urusi.

Urusi imetangaza kwamba itawaruhusu wakazi wa mikoa ya Zaporizhzhia na Kherson kuomba pasipoti ya Kirusi kupitia "utaratibu uliorahisishwa". Ukraine imeshutumu mara moja hatua inayoonyesha nia ya Moscow ya kutqaka kukalia kwa urahisi maeneo haya.

Kwa upande wa kidiplomasia, Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel amesema bado "ana imani" na makubaliano juu ya vikwazo vya EU kuhusu mafuta ya Urusi katika ufunguzi za ikao cha Baraza la Ulaya Jumatatu, licha ya kizuizi cha Hungary.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.