Pata taarifa kuu
UFARANSA

Macron aapishwa kuhudumu kwa muhula wa pili.

Rais wa Ufransa Emmanuel Macron, ameapishwa rasimi  kuhudumu kwa muhula wa pili  kufuatia ushindi wake dhidi ya mrengo wa kulia, Macron sasa anakuwa  rais wa kwanza nchini Ufaransa kuhudumu kwa muhula wa pili baada ya kipindi kwa miaka 20.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron. AP - Christophe Petit Tesson
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kuapishwa kwake kuhudumu kwa muhula wa pili wa miaka mitano, Rais Marcon anakabiliwa na changamoto za ndani na nje ya nchi ambazo anatarajiwa kubamana nazo.

Baadhi ya changamoto anazokabiliwa nazo ni pamoja na kutekeleza mageuzi aliyoahidi kufanya wakati akichaguliwa kwa awamu ya kwanza mwaka wa 2017 akiwa rais mwenye umri mdogo zaidi kuwahi chaguliwa kuongoza ufaransa.

Changamoto nyengine inayomsubiri rais huyo ni jinsi atakavyo shugulikia uvamizi uliotekelezwa na taifa la Urusi dhidi ya Ukraine.

Swala la kupanda kwa gharama ya maisha nchini mwake pia limetajwa kuwa mojawapo ya changamoto zinamzomsubiri Macron pamoja na jinsi ya kushugulikia swala la umri wafanyikazi wa umma kustaafu.

Laurent Fabius, Mkuu wa baraza la kikatiba nchini Ufransa amesoma taarifa inayodhitisha ushindi wa Macron katika duru ya pili ya uchaguzi wa tarehe 24 ya mwezi April ambapo aliibuka mshindi kwa asilimia   58.55 dhidi ya mpinzani wake wa mrengo wa kulia Marine Le Pen.

Licha ya sherehe za leo za kuapishwa kwa rais Macron kwa muhuma wa pili wa miaka mitano, Majukumu yake ofisini yanatarajiwa kuaanza rasimi baada ya kumalizika kwa muhula wake wa kwanza ifikapo usiku wa kuamkia tarehe 13 ya mwezi mei mwaka huu.

Aidha rais Macron anatarajiwa kumteua waziri mkuu mpya atayechukua nafasi ya waziri mkuu wa sasa Jean Castex wakati muhula wake wa pili utakapoaanza rasimi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.