Pata taarifa kuu

[Mubashara] vita vya Ukraine : Pande hasimu zakubaliana juu ya maeneo salama ya kiutu

Katika siku ya 56 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Kyiv imepokea ndege za kivita kusaidia kukabiliana na mashambulizi ya Urusi mashariki mwa nchi, ambapo wapiganaji wa mwisho wa Ukraine waliokuwa wamekimbilia Mariupol walitoa wito wa kukata tamaa kwa jumuiya ya kimataifa kwa kuweza kuokolewa.

Gari la jeshi la Urusi huko Mariupol, Aprili 19, 2022.
Gari la jeshi la Urusi huko Mariupol, Aprili 19, 2022. REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari vya Marekani vinasema nchi hiyo itaidhinisha msaada wa kijeshi wa dola milioni 800 kwa ajili ya Ukraine. Msaada huu unakuja chini ya wiki moja tu baada ya msaada mwingine wenye thamani ya kima sawa na hicho cha fedha kuidhinishwa kwa ajili ya nchi hiyo inayovamiwa na Urusi.

Pointi kuu

► "Tunaweza kuwa tunaishi siku zetu za mwisho, hata saa zetu za mwisho," kamanda wa askari wa Ukraine waliozingirwa huko Mariupol amesema kwenye Facebook leo Jumatano. Wizara ya Ulinzi ya Urusi imetoa wito kwa jeshi zima la Ukraine "kuweka chini silaha zao" na watetezi wa mwisho wa Mariupol kusitisha "upinzani wao usio na maana".

► Siku ya Jumanne asubuhi Urusi ilitangaza kuwa ilifanya mashambulizi kadhaa ya anga na kurusha makombora mashariki mwa Ukraine, wakianza na "vita vya Donbass" vilivyotarajiwa kwa wiki kadhaa, kulingana na Kyiv.

► Pentagon ilisema Jumanne kwamba jeshi la Ukraine lilipokea ndege za kivita za ziada na vipuri kwa ajili ya matengenezo ya ndege hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.