Pata taarifa kuu

Ukraine: Eneo la Mashariki lakumbwa na mashambulizi kadhaa, vita Donbass vyazinduliwa

Katika siku ya 55 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, macho yote yanatazama mashariki mwa nchi hiyo, ambako Moscow ilianzisha mashambulizi makubwa siku ya Jumatatu, kulingana na Rais Volodymyr Zelensky.

Askari wa Ukraine kwenye gari la kivita mashariki mwa Ukraine, Aprili 19, 2022.
Askari wa Ukraine kwenye gari la kivita mashariki mwa Ukraine, Aprili 19, 2022. REUTERS - UKRAINIAN GROUND FORCES
Matangazo ya kibiashara

Urusi imetangaza Jumanne asubuhi kuwa imefanya makumi ya mashambulizi ya anga na makombora usiku kucha mashariki mwa Ukraine, ikizindua "vita vya Donbass" vilivyohofiwa kwa wiki kadhaa, kulingana na Kyiv. "Haijalishi ni wanajeshi wangapi wa Urusi wataletwa hapa, tutapigana. Tutajilinda wenyewe,” Rais wa Ukraine alitangaza Jumatatu jioni.

Urusi inataka "kuikomboa" kijeshi Donbass, Moscow ikizingatia eneo hili la mashariki kama huru kutoka kwa Ukraine, Waziri wa Ulinzi wa Urusi amesema leo Jumanne, akishutumu nchini za Magharibi kwa "kurefusha" mzozo kwa kuwasilisha silaha huko Kyiv.

Hakuna maeneo ya usalama ya kiutu kwa raia yangeweza kutengwa leo Jumanne nchini Ukraine, kwa kukosekana kwa makubaliano na upande wa Urusi, na hii, ni kwa siku ya tatu mfululizo, ametangaza Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imetoa wito kwa jeshi zima la Ukraine "kuweka chini silaha zao" na watetezi wa mwisho wa Mariupol kusitisha "upinzani wao usio na maana". Jeshi la Urusi limesema lilifungua eneo salama la kiutu Jumanne hii ili kuwaondoa wanajeshi wa Ukraine waliopo katika eneo la viwanda la bandari ya kimkakati ya Bahari ya Azov, saa chache baada ya kuwataka wajisalimishe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.