Pata taarifa kuu

Ukraine yaapa kupambana katika vita vyake na Urusi hadi mwisho

Ukraine imeapa kuendelea kupambana na kuulinda mji wa Mauripol mpaka mwisho, baada ya muda uliokuwa umetolewa na Urusi kwa vikosi vyake kujisalimisha kukamilika.

Mtu huyu akitembea kando ya mabaki ya jengo lililoharibiwa huko Mariupol, jiji lililozingirwa na jeshi la Urusi, Aprili 17, 2022.
Mtu huyu akitembea kando ya mabaki ya jengo lililoharibiwa huko Mariupol, jiji lililozingirwa na jeshi la Urusi, Aprili 17, 2022. © REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal ametoa kauli hiyo baada ya wanajeshi wa Ukraine kutojisalimisha na kuongeza kuwa vikosi vya nchi hiyo bado vipi katika mji huo, na vitaendelea kupambana. 

Hii inakuja, huku Ukraine ikilishtumu jeshi la Urusi kwa kuwaondoa kwa nguvu watoto 150katika mji huo. 

Siku chache zilizopita, wanajeshi wa Urusi wamehamisha mashambulio yao, Mashariki mwa Ukraine, wakiwa na lengo la kudhibiti jimbo la Donbas. 

Naye rais Volodymyr Zelenskyy ameahidi kuwa nchi yake haitaruhusu eneo lake la Mashariki kuchukuliwa na Urusi, ili  kumaliza vita vinavyoendelea. 

Aidha, amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la fedha duniani IMF kuona namna ya kuisaidia nchi yake baada ya vita kukamilika. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.