Pata taarifa kuu

Ukraine: Rais Putin atoa tuzo ya heshima kwa kikosi kinachoshutumiwa mauaji Bucha

Rais wa Urusi Jumatatu alitunuku tuzo ya heshima ya "ushujaa" kwa kikosi cha 64 wanajeshi, ambacho Ukraine imekishutumu kwa kushiriki katika mauaji yaliyofanyika Bucha, karibu na Kyiv.

Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano kwa njia ya video katika ofisi yake huko Kremlin. Aprili 18, 2022.
Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano kwa njia ya video katika ofisi yake huko Kremlin. Aprili 18, 2022. via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametia saini, kulingana na Kremlin, dikri ya kutoa "jina la heshima la Walinzi" kwa kikosi hiki kwa sababu ya "ushujaa na uimara, azimio na ujasiri" wa wanajeshi wake.

Wakati huo huo jeshi la Urusi linaendelea kujizatiti katika eneo la Donbass na hasa katika jiji lililozingirwa la Mariupol. Mji wa Lviv, ambao umeepushwa na mapigano hadi sasa, umelengwa na mashambulio "makubwa" matano ya makombora, na kuua takriban watu saba na kujeruhi kumi na mmoja. Hata hivyo Rais Vladimir Putin amesema kuwa vikwazo dhidi ya Urusi vitaathiri nchi za Magharibi.

Huko Mariupol, jiji la bandari kusini-mashariki, watetezi wa mwisho wa Ukraine bado wanapigana katika baadhi ya maeneo. Wanajeshi hawa wanaonekana kupuuza kauli ya mwisho iliyotolewa na jeshi la Urusi siku ya Jumapili. "Watapigana hadi mwisho," ameonya Denys Chmygal, Waziri Mkuu wa Ukraine.

Jeshi la Urusi limedai Jumatatu jioni kuwa limeharibu kwa "makombora ya usahihi wa hali ya juu" ghala kubwa la silaha za kigeni zilizowasilishwa hivi karibuni kwa Ukraine, karibu na Lviv (magharibi). Ndege za Urusi zilifanya mashambulizi asubuhi dhidi ya kituo cha vifaa cha vikosi vya Ukraine, amesema msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi, Igor Konashenkov.

Umoja wa Ulaya siku ya Jumatatu umelaani mashambulizi ya Urusi ya kiholela na kinyume cha sheria ya makombora na milipuko ya mabomu dhidi ya raia nchini Ukraine na kukemea uhalifu wa kivita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.