Pata taarifa kuu

Kyiv, Lviv zakumbwa na mashambulizi ya Urusi

Jeshi la Urusi limeendeleza mashambulio katika kituo cha jeshi cha Ukraine jijini Kiev, hatua inayokuja baada ya kuonya hilo kufuatia madai ya Ukraine kuushambulia mji wake. 

Magari ya kijeshi ya Ukraine katika vitongoji vya Kyiv, Aprili 11, 2022.
Magari ya kijeshi ya Ukraine katika vitongoji vya Kyiv, Aprili 11, 2022. © Evgeniy Maloletka/AP
Matangazo ya kibiashara

Mashambulio haya mapya yamekuja baada ya meli ya kijeshi ya Urusi, ya kijeshi kuharibiwa na kuzama, na kuishtuu Ukraine kwa kutekeleza mashambulio katika ardhi yake na kuonya kujibu hatua hiyo kulenga jiji la Kiev. 

Meya wa mji wa Kiev Vitali Klitschko amesema mtu mmoja ameuawa  na wengine kujeruhiwa baada ya jeshi la Urusi kulenga na kushambulia kituo cha jeshi karibu na uwanja wa ndege kinachohifadhi mizinga ya kijeshi, huku mashambulio zaidi yakiripotiwa katika mji wa Lviv, Magharibi mwa Ukraine. 

Polisi jijini Kiev wanasema , miili 900 ya wakaazi wa mji huo, wamepatikana baada ya wanajeshi kuondoka siku kadhaa zilizopita. 

Rais Volodymyr Zelenskyy ameonya kuwa dunia ichukulie kwa makini tishio la Urusi kuishambulia nchi yake kwa silaha za kemikali na kumtak, mwenzake wa Marekani Joe Biden atangaze Urusi kama nchi inayounga mkono ugaidi. 

Katika hatua nyingine, serikali ya Urusi imetangaza kumzuia Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Mawaziri wake kuja nchini humo, kufuatia msimamo wa taifa hilo la Ulaya kuhusu vita vinavyoendelea nchini Ukraine. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.