Pata taarifa kuu

Ukraine: Kyiv yadai kusitisha 'mazungumzo' ikiwa askari wake wataangamizwa Mariupol

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensy ameonya Jumamosi kwamba "kuangamizwa" kwa wanajeshi wa mwisho wa Ukraine waliopo katika mji wa bandari wa Mariupol uliozingirwa na vikosi vya Urusi "kutasitisha mazungumzo ya amani" na Moscow.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa hotuba yake mnamo Machi 28, 2022.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa hotuba yake mnamo Machi 28, 2022. © Ukrainian Presidential Press Office via AP
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati Urusi imetangaza kwamba Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na maafisa wengine kadhaa wakuu wa Uingereza wamepigwa marufuku kuingia nchini humo, baada ya London kuiwekea vikwazo Moscow kutokana na operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine.

Wakati huo huo Rais wa Ukraine alisema siku ya Ijumaa jioni kwenye kituo cha televisheni cha CNN kwamba kati ya wanajeshi 2,500 na 3,000 wa Ukraine wameuawa tangu kuanza kwa mzozo kati ya Urusi na Ukraine, na kuongeza kuwa wengine 10,000 wamejeruhiwa.

Katika Donbass, watu wanaodoka katika miji na vijiji wakati mashambulizi ya Urusi yanakaribia. Huko Kramatorsk, 70% ya watu wameondoka na kukimbilia Magharibi mwa nchi. Lakini wengine wameamua kubaki, licha ya milipuko ya mabomu, uhaba wa mafuta na mapigano yanayokaribia.

“Kwa nini kuondoka? Hatujui vita hii itadumu kwa muda gani. Magharibi mwa Ukraine, hakuna kazi, hakuna pesa za kukidhi mahitaji. Chaguo jingine ni kusalia Kramatorsk na kutumaini mambo yatakuwa bora,” amesema Maxim mwenye umri wa miaka 16.

Italia yafunga bandari zake kwa meli za Urusi

Kuanzia Aprili 17, meli za Urusi zilizoegesha katika bandari za Italia zitalazimika kuanza safari baada ya kumaliza "shughuli zao za kibiashara". Mamlaka ya Italia imezuia zaidi ya euro milioni 800 za watu wa Urusi wanaolengwa na vikwazo vya nchi za Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.