Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Boris Johnson apigwa marufuku kuingia Urusi

Fuatilia moja kwa moja habari za hivi punde kuhusu mzozo wa Ukraine, Jumamosi hii, Aprili 16, siku ya 52 ya uvamizi wa Urusi.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini Kyiv Aprili 9, 2022.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini Kyiv Aprili 9, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

► Moscow imezuia tovuti ya RFI, ambayo inatangaza habari katika lugha kumi na tano ikiwa ni pamoja na Kirusi. URL mbadala inwezesha kufikia tovuti katika Kifaransa na Kirusi. RFI katika Kirusi inapatikana pia kwenye Telegraph: https://t.me/RFI_Ru, kupitia VPN na nchini Urusi kwa Kifaransa kwa satelaiti kwenye Hotbird.

Pointi kuu:

► Kiwanda cha kutengeneza mizinga ya kijeshi hasa kimelengwa Jumamosi hii asubuhi na kumeripotiwa shambulio la anga katika viunga vya mji wa Kyiv.

► Urusi imetangaza kwamba Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na maafisa wengine kadhaa wakuu wa Uingereza wamepigwa marufuku kuingia nchini humo, baada ya London kuiwekea vikwazo Moscow kutokana na operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine.

► Rais wa Ukraine alisema Ijumaa usiku kwenye CNN kwamba kati ya wanajeshi 2,500 na 3,000 wa Ukraine wameuawa tangu kuanza kwa mzozo kati ya Urusi na Ukraine, na kuongeza kuwa wengine 10,000 wamejeruhiwa.

►Kufikia Aprili 15, zaidi ya watu milioni tano wamekimbia Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi, kulingana na takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi.

Wakati huo huo, Marekani imesema inaamini makombora ya Ukraine ndiyo yaliipiga meli ya kivita ya Urusi na kusababisha uharibifu mkubwa, kinyume na madai ya Urusi kwamba uharibifu huo ulisababishwa na tukio la moto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.