Pata taarifa kuu

Vita huko Ukraine: Ukraine yaishambulia meli ya Urusi katika Bahari Nyeusi

Ukraine inadai imeshambulia meli ya kijeshi ya Urusi na kuiharibu vibaya, hatua ambayo imethibitishwa na Moscow amnbayo inasema ilichoharibu meli hiyo ni moto na inachunguza tukio hilo.

Meli kubwa ya Urusi "Moskva" katika Bosphorus ikielekea Bahari ya Mediterania, huko Istanbul, Uturuki, Juni 18, 2021.
Meli kubwa ya Urusi "Moskva" katika Bosphorus ikielekea Bahari ya Mediterania, huko Istanbul, Uturuki, Juni 18, 2021. REUTERS - YORUK ISIK
Matangazo ya kibiashara

Ukraine inasema, baada ya kuishambulia meli hiyo, ilianza kuzama, lakini Urusi imekanusha madai hayo na kusema moto ndio uliosababisha mlipuko wa meli hiyo ambayo bado inaelea.

Wakati hayo yakijiri, Meya wa mji wa pwani wa Mariupol, amesema watu zaidi ya Laki Moka, wanasubiri kuondolewa kwenye mji huo, wakati huu maafa yakiripotiwa katika mji wa Kharkiv unaoendelea kushuhudia mashambulizi kutoka kwa wanajeshi wa Urusi.

Katika hatua nyingine, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kuishtumu Urusi kuwa inaendeleza mauaji ya kimbari nchini Ukraine, huenda ikaendeleza zaidi vita vinavyoendelea. Kauli ya kuishtumu Urusi kutekeleza mauaji ya kimbari nchini Ukraine, yalitolewa na rais wa Marekani Joe Biden.

Wakati huo hu, Biden ametangaza msaada zaidi wa Dola Milioni 800 kuisaidia Ukraine kununua silaha za kuendelea kupambana na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.