Pata taarifa kuu

Urusi kuendelea kubanwa katika uvamizi wake dhidi ya Ukraine

Marekani na washirika wake, wamekubaliana kuiwekea Urusi vikwazo zaidi, wakati huu wanajeshi wake wanapoendelea kushambulia miji ya Mashariki mwa nchi ya Ukraine, huku Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akimshutulu Rais Vladimir Putin kwa uhalifu wa vita. 

Mkazi wa Mariupol akipita karibu na kifaru cha Urusi, Aprili 19, 2022.
Mkazi wa Mariupol akipita karibu na kifaru cha Urusi, Aprili 19, 2022. REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

Wakati mataifa hayo ya magharibi yakikubaliana kuhusu hilo, jeshi la Urusi linasema, limerusha makombora na kulenga vituo 13 vya kijeshi vya Ukraine katika jimbo la Donbas. 

Aidha, Urusi inawataka wanajeshi wa Ukraine walio katika kiwanda cha kutengeneza vyuma mjini Mariupol kuweka silaha chini na kujisalimisha. 

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress, ametaka vita visitishwe kwa siku nne, ili kuruhusu watu kukimbilia katika maeneo salama. 

Wakati hayo yakijiri, Mawaziri wa Fedha kutoka mataifa tajiri duniani ya G 20 wanakutana kujadili namna vita vya Ukraine na Urusi vinavyosabisha mataifa mbalimbali kuendelea kukumbwa na madeni na gharama ya  bei ya bidhaa hasa chakula. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.