Pata taarifa kuu

Vita Ukraine: Kyiv yajiandaa kwa kuanguka kwa Mariupol na kwa mashambulizi Mashariki

Katika siku ya 48 ya uvamizi wa Urui nchini Ukraine Jumanne hii Aprili 12, vikosi vya Urusi vimeendelea na shinikizo lao kwa mji wa kimkakati wa bandari wa Mariupol wakati huko mashariki, Kyiv inatarajia mashambulizi makubwa hivi karibuni.

Kombora limekwama ardhini huko Kharkiv, Aprili 11, 2022.
Kombora limekwama ardhini huko Kharkiv, Aprili 11, 2022. REUTERS - ALKIS KONSTANTINIDIS
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa waasi wanaounga mkono Urusi huko Donetsk alisema Jumatatu kwamba vikosi vyake vimelidhibiti kabisa eneo la bandari la mji wa kimkakati wa Mariupol, kusini mashariki mwa Ukraine, ambao umezingirwa kwa zaidi ya mwezi mmoja. Mwakilishi wa jeshi la waasi waliojitenga, kwa upande wake amesema kuwa wapiganaji wa mwisho wa Ukraine walikuwa wakijidhatiti kuviteka viwanda vikubwa vya "Azovstal" na "Azovmach".

Makumi ya maelfu ya watu waliuawa huko Mariupol, jiji la kusini mwa nchi lililoshambuliwa na jeshi la Urusi, kulingana na mamlaka huko Kyiv. Iwapo takwimu hizi zitathibitishwa, itakuwa ni idadi kubwa ya vifo vya watu waliorekodiwa katika mji wa Ukraine tangu Urusi ilipovamia nchi hiyo mnamo Februari 24.

Maafisa sita wa idara ya ujasusi ya Urusi wanaofanya kazi "chini ya mamlaka ya ubalozi" wametangazwa kupoteza imani yao na serikali ya Ufaransa, Quai d'Orsay ilitangaza siku ya Jumatatu.

Wakati huo huo Rais Volodymyr Zelenskiy amesema nchi yake haina silaha za kutosha zinazohitajika kuweza kuukomboa mji wa Mariupol ambao upo hatarini kudhibitiwa na vikosi vya Urusi.

Zelenskiy ametoa kauli hiyo kupitia hotuba kwa njia ya vidio akitaka ulimwengu kumsaidia silaha kama vile mizinga na ndege za kivita ili kuweza kuhimili mashambulizi ya Moscow. Amedai kwamba Urusi inaweza kutumia silaha za kemikali nchini Ukraine na kuzitaka nchi za Magharibi kuiwekea Moscow vikwazo vikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.